UNHCR yakaribisha kauli ya Kenya kuhusu Daadab

UNHCR yakaribisha kauli ya Kenya kuhusu Daadab

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekaribisha tamko la serikali ya Kenya la kusaka suluhu ya kudumu kwa wakimbizi katika kambi ya Daadab nchini humo.

Katika taarifa yake, UNHCR imegusia uamuzi huo wa serikali ya Kenya kuhusu wakimbizi wa Somalia ikisema kuwa wale wanaotaka kurejea kwa hiari Somalia watakwenda katika mazingira ya kiutu na kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Sasa UNHCR imesema ombi lake kwa Kenya ni nchi hiyo ionyeshe urejeshaji wa hiari unaoendana na mazingira, ikimaanisha kwamba ratiba isiwe ambayo haingalii mazingira yaliyopo.

Kwa mantiki hiyo imeomba wadau wote kuzingatia utekelezaji wa mpango huo ikiwemo mazingira ya ndani mwa Somalia na kwenye ukanda husika, ikitaka jamii ya kimataifa iwekeze vya kutosha Somalia ili kutoa hakikisho la amani na usalama.

Photo Credit
Wakimbizi wapya kutoka Somalia wakisubiri kusajiliwa katika kambi ya Dadaab. Picha: UNHCR/U.Hockstein