Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia kataeni wagombea ubunge wenye historia ya uhalifu

Somalia kataeni wagombea ubunge wenye historia ya uhalifu

Pakua

Jamii ya kimataifa imesema ina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti ya kwamba baadhi ya wagombea ubunge nchini Somalia wana historia ya vitendo vya uhailfu ikiwemo ugaidi.

Ofisi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM imenukuu ripoti hizo kutoka taarifa ya pamoja ya umoja huo, muungano wa Afrika, muungano wa Ulaya, IGAD, Ethiopia, Sweden, Italia, Uingereza na Marekani.

Wamesema kuwa kitendo cha kujumuishwa kwa wagombea hao, kinarudisha nyuma harakati za Somalia wakati huu ambapo nchi hiyo inajiandaa kufungua ukurasa mpya.

Wametaka wakati huu upigaji kura bunge la juu ukiendelea, wagombea wa aina hiyo wasichaguliwe, halikadhalika katika uchaguzi wa wawakilishi wa bunge la chini badaye mwezi huu.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating amesema kukataliwa kwa wagombea ubunge wenye historia chafu kutathibitisha azma ya Somalia ya kutaka kuondokana na utamaduni wa ukwepaji sheria mbele ya wananchi wake na dunia kwa ujumla.

Photo Credit
UN Photo/ Sabir Olad