Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi yakielekea Mosul, UNHCR yajiandaa na wimbi kubwa la wakimbizi

Mashambulizi yakielekea Mosul, UNHCR yajiandaa na wimbi kubwa la wakimbizi

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR linajiandaa na uwezekano wa kuwepo kwa idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani wakati huu ambapo operesheni ya kijeshi inaelekezwa mji wa Mosul.

Hali hiyo inatia hofu wakati ambapo tayari miezi ya karibuni watu zaidi ya Laki Mbili walikimbia makwao kutoka maeneo mbali mbali ya nchi kutokana na mashambulizi ya kijeshi.

Adrian Edwards ambaye ni msemaji wa UNHCR anaeleza kuwa Mosul ni mji wa pili kwa ukubwa Iraq na hivyo athari za operesheni za kijeshi zinatarajiwa kuwa kubwa na takribani watu Milioni Moja nukta mbili wanaweza kuathiriwa, kwa hiyo..

(Sauti ya Adrian)

“Tunatarajia kujenga kambi katika maeneo sita kaskazini mwa nchi na u wezekano wake unategemea upatikanaji wa ardhi na fedha na tumetoa ombi la dola Milioni 584 kwa ajili ya wakimbizi wa ndani wakiwemo wakimbizi wa Iraq kwenye eneo hilo, na ombi hili limechangiwa kwa asilimia 38 tu.”

Photo Credit
Wanawake wa Mosul. Picha: HCR/S. Baldwin (Maktaba)