Maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Afrika Mashariki

Maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Afrika Mashariki

Pakua

Maadhimisho ya miaka sabini ya Umoja wa Mataifa ni fursa ya kutafakari, na kuangalia historia na hatua ambazo Umoja wa Mataifa umepiga. Kadhalika ni fursa ya kuangazia ambapo Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa kwa ujumla inapaswa kuimarisha juhudi zake ili kukabiliana na changamoto mbali mbali kupitia kazi zake za amani, maendeleo na haki za kibinadamu. Huo ni ujumbe wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika maadhimisho hayo.

Nchi mbali mbali zinaadhimisha miaka sabini kwa njia tofauti ambako nchini Tanzania kunafanyika shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuungana na dunia katika maadhimisho hayo kwa ushirikiano na serikali ikiwemo upandaji wa miti 1000 katika mlima Kilimanjaro na hivi karibuni timu ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wamefanya usafi katika soko la Temeke mjini Dar Es Salaam .

Je ni nini kimefanyika? Basi tuungane na Amina Hassan kupata hali halisi.

Photo Credit
Usafi katika soko la Temeke jijini Dar Es Salaam.(Picha:UN/Tanzania/facebook)