Simulizi ya mwanamke aliyebakwa na kupata ujauzito wakati wa mzozo Sudan
Mwaka mmoja wa mzozo nchini Sudan umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi.
Jamii za watu wa asili wanaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi - Samante Anne
Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira, nilipata fursa ya k
Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”
Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania
Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali.
Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili
Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani.
(Taarifa ya Anold Kayanda)
Mtu 1 kati ya 5 katika nchi 59 duniani anahitaji hatua za haraka kuepushwa na baa la njaa: FAO
Ripoti mpya ya kimataifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuhusu mgogoro wa chakula duniani inasema karibu watu milioni 282 walio katika nchi 59 walikabiliwa na viwango vya juu vya njaa mwaka 2023.
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
24 APRILI 2024
Karibu kusikiliza jarida hii leo linaangazia masuala mbalimbali ikiwemo ripotoi ya mgogoro wa chakula duniani, kuanza kwa wiki ya chanjo na utoaji chanjo kwa watoto mashinani.
23 APRILI 2024
Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP.