Tunawapatia vijana stadi za kujikwamua kama kusuka nywele na ushoni- FPMHE
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mashirika ya kiraia yamekuwa yakiunga mkono harakati za kukwamua vijana kutoka katika madhila mbalimbali ikiwemo umaskini. Hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba vita nchini humo vimesababisha vijana wa kike na wa kiume kujitumbukiza kwenye mambo
Bei ya vyakula imepanda
Kuagiza chakula kutoka nje kunaongeza mzigo mkubwa kwa mataifa maskini duniani, imesema ripoti mpya kuhusu hali ya chakula iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa la FAO.
Huduma ya vitambulisho vya kidijitali ni mkombozi wa wanawake Uganda
Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia zaidi ya watu bilioni 1.1 duniani hawana vitambulisho rasmi kitu ambacho kinawanyima wengi fursa muhimu katika huduma za kijamii na za kimaendeleo.
Takwimu za kuanzia kaya hadi taifa ni muarobaini wa kupambana na umaskini- Balozi Mushi
Mkutano wa ngazi ya juu wa kutathmini utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ukiendelea jijini New York, Marekani, Tanzania imesema kama ilivyo kwa nchi nyingine, takwimu sahihi ndio kikwazo kikubwa cha utekelezaji wa ahadi hiyo ambayo ilipitishwa mwaka 2015.
Dunia imeshindwa kunusuru watoto- UNICEF
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio linalotoa muongozo wa namna ya kulinda haki, usalama na ustawi wa watoto walioko ndani ya mzunguko wa mizozo, pamoja na kuimarisha juhudi za kujenga amani endelevu.
Walinda amani wa Afrika wanalinda dunia nzima- Guterres
Umoja wa Mataifa, UN na Muungano wa Afrika, AU wameelezea wasiwasi wao mkubwa juu ya sintofahamu inayoendelea kukumba mfumo wa dunia na kusababisha madhara kwenye amani na usalama duniani.
Marufuku ya matumizi ya plastiki Uganda yasuasua
Idadi kubwa ya mifuko ya Plastiki inayotumika katika nchi nyingi duniani husususan nchi zinazoendelea ina madhara kwa ardhi, mito, baharí kutokana na kuwa haiozi.
Kutana na wavuvi wanawake nchini Chad
Changamoto za mabadiliko ya tabianchi na udhibiti mbaya wa maji , vinawaweka roho juu wanawake wavuvi nchini Chad ambao mlo na maisha yao ya kila siku hutegemea uvuvi, sasa samaki wameanza kuadimika na kuwaongezea mtihani wa kiuchumi na kijamii. Flora Nducha na taarifa kamili
Tanzania na mpango shiriki wa uhifadhi wa misitu
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya misitu duniani imezitaka serikali kuchukua hatua jumuishi katika ulinzi na uhifadhi wa misitu ili kupunguza kasi ya kupungua kwa eneo la misitu kila uchao.