Demokrasia duniani iko njia panda- Ripoti
Demokrasia duniani iko njia panda na hatua lazima zichukuliwe ili kuilinda na kuiheshimu, imesema ripoti ya kwanza iliyozinduliwa leo huko Geneva, Uswisi kuhusu hali ya demokrasia ulimwenguni.
Demokrasia duniani iko njia panda na hatua lazima zichukuliwe ili kuilinda na kuiheshimu, imesema ripoti ya kwanza iliyozinduliwa leo huko Geneva, Uswisi kuhusu hali ya demokrasia ulimwenguni.
Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limepokea zaidi ya dola milioni 2.3 kutoka Ujerumani ili kusaidia upatikanaji wa chakula kwa takribani wakimbizi nusu milioni walioko Tanzania na Rwanda.
Idadi ya wagonjwa wa Malaria kwa mwaka 2016 iliongezeka kwa zaidi ya visa milioni 5 ikilinganishwa na mwaka 2015 na hivyo kutiwa hofu juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kutokomeza ugonjwa huo.
Nchini Costa Rica sera ya kuwezesha wakimbizi kufanya kazi imeleta nuru kwa raia wa Colombia waliokimbia machafuko nchini mwao. Flora Nducha na ripoti kamili.
(Taarifa ya Flora Nducha)
Takribani aina moja ya dawa kati ya 10 zinazotumika katika nchi za kipato cha chini na kati ni bandia au hazijakidhi viwango.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya uliotolewa leo na shirika la afya ulimwenguni, WHO.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kujadili wapiganaji mamluki wanaojiunga na vikundi vya kigaidi, jambo ambalo linatishia amani na usalama duniani.
Upatikanaji wa mikopo ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa sekta binafsi na mabadiliko ya kiuchumi barani Afrika. Hata hivyo, utafiti uliofanyika nchini Kenya umeonyesha kwamba akiba hazikukua kwa kasi iliyotakiwa ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wafanya biashara.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu huko mjini Roma Italia, yameazimia kushirikiana ili kutokomeza njaa katika nchi masikini kwa mujibu wa ajenda ya 2030.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Ján Kubiš amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea usiku wa kuamkia leo kwenye mji mkuu Baghdad na kusababisha vifo vya raia 12 na kujeruhi wengine wengi.
Mhandisi kijana kutoka Yemen Omer Badokhon leo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya bingwa wa uhifadhi wa mazingira duniani.