Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP, IFAD na FAO wachukua hatua kutokomeza njaa ifikapo 2030

WFP, IFAD na FAO wachukua hatua kutokomeza njaa ifikapo 2030

Pakua

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu huko mjini Roma Italia, yameazimia kushirikiana ili kutokomeza njaa katika nchi masikini kwa mujibu wa ajenda ya  2030.

Mashirika hayo ni lile la mpango wa chakula duninai WFP, lile la chakula na kilimo FAO na lile la kimataifa la maendeleo ya kilimo IFAD ambapo leo wamewasilisha mpango watakaojadili ili kuimarisha ushirikiano huo.

Naibu Mkurugenzi wa IFAD Dongxin Feng amesema hayo wakati wa tamasha la nchi zinazoendelea, zijulikanazo pia kama ushirikiano wa kusini-kusini huko Antalya, Uturuki.

Amesema kwa kuzingatia mamlaka ya kila shirika na fursa na uwezo walio nao katika kufanikisha uhakika wa chakula na kuboresha kilimo, wataweza kuwa na ufanisi zaidi iwapo watashirikiana na kusongesha mbinu bunifu na rahisi ili kufanikisha ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.

Naye Ashwani Muthoo mkurugenzi katika idara ya IFAD  amesema imethibitishwa kuwa mfumo wa kutoa huduma unaopatia kipaumbele michango ya kupunguza pengo la huduma ni bora na thabiti hivyo ushirikiano miongoni mwa mashirika hayo ni sahihi.

Photo Credit
Mtoto Ahmed mwenye umri wa miaka mitatu apokea matibabu dhidi ya utapiamlo.(Picha:WFP/Abeer Etefa)