Kutoka kulala mitaani hadi kumiliki duka la mikate Costa Rica
Nchini Costa Rica sera ya kuwezesha wakimbizi kufanya kazi imeleta nuru kwa raia wa Colombia waliokimbia machafuko nchini mwao. Flora Nducha na ripoti kamili.
(Taarifa ya Flora Nducha)
Miaka 17 iliyopita, ghasia nchini Colombia zilisababisha Miriam Velásquez na mumewe Ricardo Ángel kukimbia nchi yao na kusaka hifadhi nchini Costa Rica.
Baada ya kuwasili kwenye mji mkuu San Jose, familia hiyo haikuwa na kipato chochote na hivyo kujikuta wanaishi mitaani.
Hata hivyo hivi sasa maisha yao yamebadilika baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kuwapatia mtaji kidogo wa kufungua duka la kuoka mikate isiyo na protini.
Miriam anasema maisha yao yamebadilika.
(Sauti ya Miriam Velásquez)
“Tulikuja na ari na bado tuna ari hiyo ya kuhangaika ili tufanye chochote, tufanye kazi na kusonga mbele.”

(Sauti ya Miriam Velásquez)
“Bila shaka hiki tulichofanya kinaweza kuwa mfano kwa wengine.”