Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya FAO/ILO yataniwezesha kupanga bei sahihi ya mazao- mnufaika wa mafunzo

Mafunzo ya FAO/ILO yataniwezesha kupanga bei sahihi ya mazao- mnufaika wa mafunzo

Pakua

Elimu ya Biashara imekuwa na faida kubwa kwa wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na kilimo, ikiwemo wakulima wadogo wadogo, vijana, wanawake, na wasimamizi wa mashamba ya uzalishaji mbegu mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Kwa kutambua hilo, washiriki kutoka wilaya za mkoa huo chini ya Mradi wa Pamoja Kigoma (KJP) awamu ya Pili)  wakiwemo Vijana, wanawake, wasimamizi wa mashamba toka gereza la Ilagala huko Uvinza na kambi ya jeshi la kujenga Taifa kikosi cha 824 Kanembwa huko Kakonko walipata fursa ya kupata mafunzo ya kuendesha miradi kibiashara yaliyofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kupitia KJP. Je nini ambacho washiriki waliondoka nacho? Assumpta Massoi wa Idhaa hii anakufafanulia zaidi kwenye makala hii.

Audio Credit
Bosco Vincent/Assumpta Massoi
Sauti
4'8"
Photo Credit
FAO Tanzania