Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 APRILI 2024

02 APRILI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika harakati za kuwainua wanawake na wasichana nchini Tanzania Tanzania, ambapo Paulina Ngurumwa kutoka KINNAPA Development Programme, shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara anazungumza na Anold Kayanda wa idhaa hii. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.

  1. Leo maafisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wa misaada 7 wa shirika lisilo la kiselikali au NGO la World Central Kitchen yaliyofanywa na jeshi la Israel, maafisa hao wakirejea kueleza hofu yao kwamba hakuna mahali palipo salia kuwa salama Gaza.
  2. Tume ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya UNJHRO imesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC. 
  3. Leo ni siku ya kimataifa ya kuelimishana kuhusu usonji maudhui yakiwa kutoka kuishi kuelekea kwenye ustawi, kwa watu wenye usonji au kwa kiingereza Autism, ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, usonji hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani.
  4. Na mashinani tunaelekea Gaza kuona ni kwa jinsi gani mashambulizi ya Israel ya hivi majuzi yameathiri huduma za afya katika hospitali ya Al-Shifa.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'38"