Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini kugawanyika kwa misingi ya kikabila kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe: UNMISS

Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini inaendelea kuorodhesha ukiukaji wa haki za binadamu.
UN Photo/Isaac Billy
Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini inaendelea kuorodhesha ukiukaji wa haki za binadamu.

Sudan Kusini kugawanyika kwa misingi ya kikabila kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe: UNMISS

Haki za binadamu

Vita mbili za wenyewe kwa wenyewe viwili Sudan Kusini zimeigawanya  nchi hio kikabila  huku raia wakiathirika  zaidi na ghasia, matukio ambayo yameambatana na uvunjaji mkubwa wa haki za kimataifa za binadamu za na sheria ya  kimataifa ya kibinadamu.

Akiongea mjini Juba katika jukwaa lilioandaliwa na tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani, mkurugenzi wa kitengo cha Umoja wa Mataifa Idara ya haki za kibinadamu ya katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, Musa Gassama, amesema  kwamba licha ya juhudi zote za kukuza haki za kibinadamu, taifa hili linakumbwa na changamoto kuanzisha Kwenye mfumo wa wa haki na jinai  usio na ufanisi.

Akiwalenga washiriki kutoka taasisi tofauti za za haki, Gassama amesema “ "Kuhakikisha uwajibikaji ni muhimu kwa kuunda jamii yenye haki na usawa ambapo haki za binadamu zinaheshimiwa na kulindwa, pamoja na haki kwa waathirika na jamii zilizokumbwa na migogoro." 

Kwa mujibu wa kanuni za Haki za Binadamu za Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, kuna haja ya kuimarisha uwezo wa taasisi za haki za binadamu, maafisa wa serikali, mashirika ya kiraia na watetezi wa haki za binadamu. 

Rais wa Sudan Kusini wakirejea nyumbani baada ya kuzuka machafuko Sudan
© UNMISS/Peter Bateman
Rais wa Sudan Kusini wakirejea nyumbani baada ya kuzuka machafuko Sudan

Vile vile amesisitiza umuhimu wa kuunga mkono utawala wa sheria kama mahakama, polisi na magereza.

Ameongeza kuwa "Mafunzo haya yanakusudia kuimarisha utendakazi wa wahusika wa maswala ya haki na mashirika ya kiraia ili kuchunguza, kutafiti, kuweka kumbukumbu, na kusaidia juhudi za kuripoti uvunjaji wa haki za binadamu na unyanyasaji, na pia kuboresha mifumo ya uwajibikaji nchini Sudan Kusini." 

Kwa upande wake Waziri, wa Mambo ya Ndani nchini humo Angelina Teny,  amesema, "Sisi, tulio katika sekta tunatambua kuwa kutunga sheria kwa mtindo wa ndani ni muhimu sana, ambayo inamaanisha lazima tuchunguze na kufanya uchambuzi wa kile kilicho katika nchi yetu kwa kuhakikisha kwamba uvunjaji wa haki za binadamu unashughulikiwa kitaifa."

Mwakilishi wa Shirikisho la Mawakili Wanawake nchini humo Debora Ezbon naye akaongeza kwa kusema kuwa,"Mafunzo haya yamekuja wakati muhimu ambapo mfumo wa haki pamoja na uvunjaji wa haki za binadamu na unyanyasaji bado umekithiri Sudan Kusini."