Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya vitendo yaleta afuweni kwa wakimbizi na raia kwenye makazi ya Kalobeyei Kenya:UNHCR

Fundi cherehani raia wa Jamhuri wa Kidemokrasi ya Congo- DRC lakini akiishi kama mkimbizi Kenya.
© UNHCR/Rose Ogola
Fundi cherehani raia wa Jamhuri wa Kidemokrasi ya Congo- DRC lakini akiishi kama mkimbizi Kenya.

Mafunzo ya vitendo yaleta afuweni kwa wakimbizi na raia kwenye makazi ya Kalobeyei Kenya:UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Mafunzo ya vitendo yanayotolewa kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwenye makazi ya Kalobeyei yameinua matumaini ya maelfu ya wakimbizi na raia wa Kenya katika eneo hilo.

Makazi hayo yaliyo nje kidogo ya kambi kubwa kabisa ya wakimbizi ya Kakuma yameshuhudia wakimbizi na raia wa Kenya wakifaidika kwa ujuzi wa aina mbalimbali unatolewa na UNHCR kwa ufadhili wa baraza la wakimbizi la Denmark kupitia mfuko wa hisani wa Muungano wa Ulaya (EUTF)

Mafunzo hayo ni ya aina mbalimbali kuanzia ushonaji, ufundi bomba na hata ufundi umeme.

NATTS…..

Akiwa kazini ni Batamutiza Mariya mkimbizi kutoka Congo DRC, amefuzu mafunzo hayo na sasa ni fundi bomba

( SAUTI YA BATAMUTIZA  MARIYA)

Yeye ni miongoni mwa wakimbizi na raia wa Kenya 300 waliofaidika akiwemo mkimbizi kutoka Burundi Beatrice Silas Kasimba aliyehitimu mafunzo ya ushoni

(SAUTI YA BEATRICE KASIMBA)

Wahitimu wengi wameshaanza kufaidika na mafunzo hayo. Godfrey Okumu John amemaliza mafunzo ya umeme

(SAUTI YA GODFREY OKUMU)

“Kwa ujuzi huu nitaweza kwenda nje na kutafuta kazi”

Mafunzo yote haya yanahakikiwa na mamlaka ya taifa ya mafunzo nchini Kenya (NITA) kabla ya vyeti kiutolewa. Naye Kashindi Siyaona mkimbizi kutoka DRC , anatarajia kupata cheti chake hivi karibuni akihitimu mafunzo ya urembo wa nywele.

Wanafunzi wa kwanza 303 wa mafunzo hayo wamefanya mtihani wa kuhitimu Disemba mwaka jana kutoka kwenye makazi ya Kalobeyei ambayo yana jumla ya wakimbizi 38,000.