Waandishi wa habari 400 Afrika Magharibi wamepatiwa mafunzo na IOM

8 Februari 2019

Ripoti sahihi, dhahiri na zilizoandikwa kwa ufasaha kuhusu wahamiaji zina wajibu muhimu wa kuelimi Afrika Magharibi kuhusu uhamiaji wakiholela na katika kuwajumuisha tena kwenye jamii wahamiaji wanaorejea katika jamii zao limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Wakiwa na jukumu muhimu la kuelimisha jamii katika nchi ambazo kiwango cha kutosoma kinakaribia asilimia 60, waandishi wa habari kwa mujibu wa IOM hawana fursa au wana fursa finyu ya mafunzo isipokuwa katika nchi zilizo na kipato cha juu kama Senegal na Nigeria.

Na kwa kulitambua hilo IOM kwa ufadhili wa mfuko wa dharura wa Muungano wa Ulaya kwa ajili ya msaada Afrika (EUTF) wiki hii imeandaa mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari ya kuripoti kuhusu uhamiaji na waandishi 28 kutoka Guinea-Bissau wamepata bahati ya kushiriki mafunzo hayo.

Waandishi hao wengi ni kutoka katika vituo vya Redio katika nchi ambayo vyombo vya habari vya magazeti sio vingi. Na mafunzo hayo yameanza na misingi ya uandishi wa habari za uhamiaji , kwanza kwa kupewa mtazamo wa hali halisi ya uhamiaji nchini Guinea-Bissau pamoja na safari za hatari za kupitia Mediteranea ya Kati na Magharibi.

Mafunzo hayo pia yanajumuisha utafiti wa kina wa lugha na maneno yanayotumika katika uhamiaji na athari za kisheria za kutumia kila neon kwa mfano “kila mkimbizi ni muhamiaji lakini sio kila muhamiaji ni mkimbizi” ikifuatia na ufafanuzi wa usafirishaji haramu wa binadamu nchini humo na sehemu zingine katika Ukanda huo.

Washiriki wa mafunzo hayo wameyazungumzia kama ni mwangaza mzuri kwao kufahamu masuala ya uhamiaji na jinsi ya kufikisha taarifa kwa jamii ambapo wamesama sasa wametambua kwa wahamiaji hata kama wana taarifa kuhusu uhamiji wengi hawajui hatari zinazoambatana na suala hilo.

Katika mafunzo hayo pia waandishi wamekumushwa kukumbatia maadili ya uandishi kila wanapotoa taarifa zao na umuhimu wake hasa kwa uhamiaji maadili yana jukumu kubwa la kuzuia na kuwalinda waathirika wa usafirishaji haramu.

Wanufaika pia wamesema wamejifunza mengi ikiwemo kuripoti habari za uhamiaji kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu na mafunzo hayo yatabadili jinsi wanavyoandika na kuripoti habari hizo.

Tangu mwaka 2018 IOM imeshatoa mafunzo kwa waandishi wa habari 400 kutoka nchi saba za Magharibi na katikati mwa Afrika ili kuimarisha uwezo wao wa kuripoti kuhusu masuala ya uhamiaji.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter