Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gaza: Sheria ya kimataifa haiwezi kutumia kwa kuchagua - Tor Wennesland

Tor Wennesland, Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati akihutubia Baraza la Usalama
UN Photo/Eskinder Debebe
Tor Wennesland, Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati akihutubia Baraza la Usalama

Gaza: Sheria ya kimataifa haiwezi kutumia kwa kuchagua - Tor Wennesland

Amani na Usalama

Mgogoro mbaya huko Gaza umeendelea, pamoja na vurugu za kila siku katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, amesema Tor Wennesland, Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati akihutubia Baraza la Usalama leo (26 Machi) jijini New York, Marekani.

Pia amesema, "Katika Gaza, athari za kibinadamu za uhasama zimekuwa mbaya na zinazidi kuwa mbaya kila siku. Takriban watu milioni 1.7 wameyakimbia makazi yao, huku takriban milioni 1 wakipewa hifadhi huko Rafah. Zaidi ya watu milioni moja huko Gaza wanatarajiwa kukabiliwa na kiwango kikubwa cha uhaba wa chakula ifikapo mwisho wa Mei, na njaa katika eneo la kaskazini mwa Gaza inakaribia, kulingana na uchambuzi wa hivi karibuni wa IPC. Hakika, vifo vinavyotokana na njaa tayari vimeripotiwa.”

Wennesland amelieza Baraza kuwa ukanushaji wa karibu kila siku wa Israeli na ucheleweshaji wa harakati zilizoratibiwa ikiwa ni pamoja na kuwekwa kizuizini kwa wafanyakazi wa kibinadamu na mifumo isiyofaa ya utatuzi na ukosefu wa idhini ya vifaa vya kutosha vya mawasiliano na magari ya kivita unafanya kazi ya kibinadamu kuwa hatari sana. Misafara ya misaada inaendelea kukabiliwa na mashambulizi, barabara kuharibika, na makundi ya watu wasiotawaliwa, huku kukiwa na ombwe la usalama. Baadhi ya maendeleo yalifanywa kwenye ukanda wa baharini kutoka Cyprus, na shehena ya kwanza iliwasili tarehe 15 Machi, pamoja na kufunguliwa kwa eneo la ufikiaji kaskazini mwa Gaza.

Amesisitiza kwamba, "Sheria ya kimataifa ya kibinadamu haiwezi kutumika kwa kuchagua. Inatumika kwa wahusika wote kwenye mzozo wakati wote na jukumu la kufuata halitegemei usawa. Ninaomboleza wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliouawa huko Gaza. Ujasiri na kujitolea kwao havitasahaulika. Kutokiuka kwa majengo ya Umoja wa Mataifa lazima kuheshimiwe wakati wote."

"Nimesalia kusikitishwa sana na upanuzi usiokoma wa makazi ya Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki. Upanuzi wa maeneo ya makazi, ikiwa ni pamoja na vituo vya nje, unazidisha uvamizi huo, huku ukizuia kwa kiasi kikubwa zoezi la watu wa Palestina haki yake ya kujitawala. Nasisitiza kwamba makazi yote ya Waisraeli katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki, hayana uhalali wa kisheria na yanakiuka sheria za kimataifa.” Amesisitiza Tor Wennesland.