Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gaza: Tutaendea vipi na usaidizi kiwa misaada kila wakati iko kwenye tishio? – Mkuu wa OCHA

Watoto katika makazi ya Muda Gaza
© UNRWA
Watoto katika makazi ya Muda Gaza

Gaza: Tutaendea vipi na usaidizi kiwa misaada kila wakati iko kwenye tishio? – Mkuu wa OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Kukiwa na ripoti za kwamba leo Wapalestina 6 wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 83 wakijeruhiwa wakati wakisubiri malori ya misaada huko Gaza, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Martin Griffiths kupitia ukurasa wa mtandao wa X ametoa wito wa kulindwa kwa operesheni za misaada ya kibinadamu inayohitajika sana Gaza.

Kabla ya tukio la leo, pia jana Jumatano kulifanyika shambulio la bomu katika ghala na kituo cha usambazaji chakula kusini mwa Rafah ambalo liliua mfanyakazi mmoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) na kuwajeruhi wengine 22.

"Ni habari za kusikitisha kwa wenzetu huko Gaza ambao tayari wamepata hasara nyingi, na kwa familia walizokuwa wakijaribu kusaidia. Tutadumishaje shughuli za misaada wakati timu zetu na vifaa viko chini ya tishio kila wakati? Lazima walindwe. Vita hii lazima ikome.”

Picha za kutisha kutoka kwenye ghala hilo zilionesha sanduku la vifaa likiwa na damu karibu na lango la kituo hicho. Lakini kulikuwa na uharibifu mdogo kwa misaada ambayo bado ilikuwa katika hatua ya kusambazwa.

Mpango wa misaada ya baharini

Katika jambo linalohusiana na hilo, meli ya Shirika lilsilo la Kiserikali la World Central Kitchen yenye jina Open Arms imesalia katika ufuo wa Gaza leo Alhamisi Machi 14 baada ya kuondoka kusini mwa Cyprus siku ya Jumanne, kwenye njia mpya ya usambazaji misaada kwa njia ya bahari. Lengo ni kufikisha tani 200 za msaada kaskazini mwa Gaza.

Mpango wa 'Visiwa vya kibinadamu' ni mbaya inaonya UNRWA

UNRWA pia imeonya kwamba mipango iliyoripotiwa ya Israeli ya kuhamisha Wapalestina milioni 1.4 kutoka mji wa kusini mwa Gaza hadi kwenye kambi au kile kinachoitwa "visiwa vya kibinadamu" kaskazini zaidi itakuwa ‘hatari kupindukia.’