Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa ufupi: Gaza, Sudan, CSW68

Kupungua kwa misaada inayoingia Gaza kwa asilimia 50 mwezi Februari kumesababisha ongezeko kubwa la utapiamlo na njaa.
© UNRWA
Kupungua kwa misaada inayoingia Gaza kwa asilimia 50 mwezi Februari kumesababisha ongezeko kubwa la utapiamlo na njaa.

Habari kwa ufupi: Gaza, Sudan, CSW68

Amani na Usalama

Meli iliyosheheni misaada ya kibinadamu imeanza safari yake kutoka Cyprus kuelekea Gaza ikiwa na shehena ya tani 200 za misaada ya kuokoa maisha kwa ajili ya wananchi wa Gaza. 

Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limeripoti lori lililosheheni misaada limekataliwa kuingia Gaza kutokana na kuwa na mikasi kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji watoto. 

Israel imeongeza mikasi imeongezwa kwenye orodha ya vitu vinavyozuiliwa kuingia Gaza.

Sudan 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP hii leo linaonya kuwa litalazimika kusitisha misaada ya kuokoa maisha nchini Chad ifikapo mwezi ujao wa Aprili iwapo litakosa ufadhili wa haraka kwa ajili ya kusaidia wakimbizi.

Onyo hilo kali linakuja wakati maelfu ya wakimbizi wa Sudan wakiendelea kumiminika kuvuka mpaka kutoka Darfur, na wakati msimu wa mvua ukikaribia kuanzia na hivyo kutishia kukatika kwa mawasiliano ya kwa ajili ya utoaji wa misaada ya kibinadamu kwenye kambi za mashariki mwa nchi ambako mamilioni ya wakimbizi i kutoka Sudan wanasaka hifadhi eneo hilo. 

Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani

Na mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, ukiendelea hapa jijini New York Marekani hii leo kutakuwa na mikutano ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo hali ya wanawake nchini Afghanistan, kuziba pengo la kujinsia kwenye elimu, athari za umaskini na uhalifu katika huduma ya utoaji mimba pamoja na mkutano wa kuangalia jinsi mabunge yanayozingatia jinsia katika kuendeleza usawa wa kijinsia ili kumaliza umaskini.