Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa ajira duniani kuongezeka 2024 sanjari na pengo la usawa: ILO

Wafanyakazi wasio na ajira wanasubiri fursa za ajira huko Lilongwe, mji mkuu wa Malawi.
© ILO/Marcel Crozet
Wafanyakazi wasio na ajira wanasubiri fursa za ajira huko Lilongwe, mji mkuu wa Malawi.

Ukosefu wa ajira duniani kuongezeka 2024 sanjari na pengo la usawa: ILO

Ukuaji wa Kiuchumi

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO kuhusu mtazamo wa ajira na kujamii imeonya juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kimataifa kwa mwaka huu wa 2024, sanjari na ukosefu wa usawa na kudumaa kwa uzalishaji hali ambayo inaibua wasiwasi.

Ripoti hiyo “Mienendo ya mtazamo wa Dunia wa ajira na kijamii 2024-WESO Trends” inasema ingawa matarajio ya kimataifa sio mazuri sana lakini kiwango cha kutokuwa na ajira na pengo la ajira vyote vimeshuka chini ya ilivyokuwa kabla ya janga la coronavirus">COVID-19 kwani masoko ya ajira yameonyesha mnepo wa kushangaza licha ya kuzorota kwa hali ya kiuchumi, hata hivyo ILO inasema kujikwamua kutokana na janga la coronavirus">COVID-19 bado hakujawa sawa kutokana na udhaifu mpya na migogoro mingi ambayo inapunguza matarajio zaidi ya haki ya kijamii.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya kiwango cha ukosefu wa ajira na kiwango cha pengo la ajira ambavyo ni idadi ya watu wasio na kazi na walio na nia ya kupata kazi vyote vimeshuka.

Wafanyakazi wanatekeleza jukumu lao katika kiwanda cha uzalishaji nchini Ethiopia.
ILO Photo/Marcel Crozet
Wafanyakazi wanatekeleza jukumu lao katika kiwanda cha uzalishaji nchini Ethiopia.

Kiwango cha ajira 2023

Ripoti hiyo ya ILO inasema kiwango cha kimataifa cha ukosefu wa ajira kwa mwaka 2023 kilikuwa ni asilimia 5.1 kikiwa kimeimarika kidogo kutoka asilimia 5.3 mwaka 2022.

Hata hivyo ripoti inasema kuimarika huko kunaanza kukumbwa na changamoto na inatabiri kwamba soko la ajira na ukosefu wa ajira duniani kote vitakuwa viaya zaidi.

“Mwaka huu wa 2024 wafanyikazi milioni mbili zaidi wanatarajiwa kutafuta kazi, na hivyo kuongeza kiwango cha ukosefu wa ajira duniani kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023 hadi asilimia 5.2. Mapato yanayoweza kutumika yamepungua katika nchi nyingi Tajiri duniani za G20 na, kwa ujumla, mmomonyoko wa viwango vya maisha unaotokana na mfumuko wa bei hauna uwezekano wa kutengamaa haraka".

Zaidi ya hayo, ripoti inasema tofauti muhimu zinaendelea kati ya nchi za kipato cha juu na cha chini. 

Wakati kiwango cha pengo la ajira mwaka 2023 kilikuwa asilimia 8.2 katika nchi zenye kipato cha juu, kilisimama kwa asilimia 20.5 katika kundi la watu wenye kipato cha chini. Vile vile, wakati kiwango cha ukosefu wa ajira cha 2023 kiliendelea kuwa asilimia 4.5 katika nchi za kipato cha juu, kilikuwa asilimia 5.7 katika nchi za kipato cha chini.

Umasikini kuendelea

Aidha ripoti hiyo inasema umaskini wa kufanya kazi una uwezekano wa kuendelea. 

Licha ya kupungua kwa haraka baada ya mwaka 2020, idadi ya wafanyakazi wanaoishi katika umaskini uliokithiri  anbao wanaopata chini ya dola 2.15 kwa kila mtu kwa siku katika masharti ya usawa wa uwezo iliongezeka kwa takriban watu milioni 1 mwaka 2023.

 

Pia idadi ya wafanyakazi wanaoishi katika umaskini wa wastani wakipata chini ya dola 3.65 kwa siku kwa kila mtu katika masharti ya PPP iliongezeka kwa watu milioni 8.4 mwaka 2023. 

Ripoti imeonya kwamba ukosefu wa usawa wa mapato umeongezeka, na pia mmomonyoko wa mapato, "vinaashiria hali mbaya kwa mahitaji ya jumla na kujikwamua kwa uendelevu zaidi kiuchumi.” 

Viwango vya kazi zisizo rasmi pia vinatarajiwa kubaki tulivu, vikikaribia asilimia 58 ya wafanyikazi wa kimataifa kwa mwaka huu wa 2024.

Ushiriki katika soko la ajira

Kwa mujibu wa ripoti kumeendelea kuwa na tofauti katika ushiriki kwenye soko la ajira katika makundi mbalimbali ambapo ushiriki wa wanawake umejikwamua haraka ingawa pengo la usawa limeendelea kukita mizizi hususani katika nchi zinazoibukia na zinazoendelea.

Kuhusu ukosefu wa ajira kwa vijana ripoti inasema umeendelea kuwa changamoto huku idadi ya watu wanaoelezwa kutokuwa katika ajira, elimu au mafunzo yaani NEET imesalia kuwa katika viwango vya juu hususan miongoni mwa wasichana na kuwa tishio kwa matarajio ya muda mrefu ya ajira.

Aidha ripoti hiyo pia imegundua kuwa watu ambao wameingia tena katika soko la ajira baada ya janga la COVID-19 hawafanyi kazi idadi sawa ya na saa walizokuwa wakifanya hapo awali na idadi ya siku za ugonjwa zinazochukuliwa zimeongezeka sana. 

Ukuaji wa tija ulipungua Baada ya ongezeko fupi la baada ya janga la ongezeko la tija ya kazi imerejea katika kiwango cha chini kilichoonekana katika muongo uliopita. Muhimu zaidi, ripoti hiyo pia inagundua kuwa licha ya maendeleo ya kiteknolojia na kuongezeka kwa uwekezaji, ukuaji wa tija umeendelea kupungua.

Vijana nchini Haiti wana ujuzi unaohitajika ili kupata kazi katika viwanda vya nguo.
© ILO/Marcel Crozet
Vijana nchini Haiti wana ujuzi unaohitajika ili kupata kazi katika viwanda vya nguo.

Uzalishaji nao umepungua

Kwa mujibu wa ripoti uzalishaji wenye tija nao ulipungua baada ya ongezeko kwa muda mfupi la baada ya janga la COVID-19 sasa umemerejea katika kiwango cha chini kilichoonekana katika muongo uliopita. 

Muhimu zaidi, ripoti hiyo pia imebaini kwamba licha ya maendeleo ya kiteknolojia na kuongezeka kwa uwekezaji, ukuaji wenye tija umeendelea kupungua.

Na inasema sababu moja ya hilo ni kwamba “kiasi kikubwa cha uwekezaji kilielekezwa kwenye sekta zisizo na tija kama vile huduma na ujenzi. Vikwazo vingine ni pamoja na uhaba wa ujuzi na kutawala kwa ukiritimba mkubwa wa kidijitali, jambo ambalo linazuia kuhamishwa kwa teknolojia kwa kasi, hasa katika nchi zinazoendelea na kuwepo kwa sekta zilizo na makampuni mengi yenye tija ndogo.”

Ripoti hii inaangalia nyuma ya takwimu za soko la ajira na kile kilichobainika na hivyo inasema lazima iwe ni sababu kubwa ya kutia wasiwasi.

Mkurugenzi mkuu wa ILO Gilbert F. Houngbo amesema “Inaanza kuonekana kana kwamba kukosekana kwa usawa huku si sehemu tu ya kujikwamua na janga la COVID-19 bali ni suala la kimuundo. Changamoto za wafanyakazi inazotambua ni tishio kwa maisha ya watu binafsi na biashara na ni muhimu kuzishughulikia kwa ufanisi na haraka.”

Ameongeza kuwa kuporomoka kwa viwango vya maisha na tija dhaifu pamoja na mfumuko wa bei unaoendelea hutengeneza mazingira ya kutokuwepo usawa zaidi na kudhoofisha juhudi za kufikia haki ya kijamii. 

Amesisitiza kuwa “Na bila uadilifu mkubwa wa kijamii kamwe hatutakuwa na ahueni endelevu”.