Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia ijikwamue na COVID-19 kwa uchumi sawia, wenye mnepo na unaojali mazingira:UN

Wafanyikazi wa jamii huko Bangladesh wanafanya kaziya kusambaza vifurushi vya usafi na kukuza uhamasishaji wa kuzuia coronavirus.
UNDP/Fahad Kaizer
Wafanyikazi wa jamii huko Bangladesh wanafanya kaziya kusambaza vifurushi vya usafi na kukuza uhamasishaji wa kuzuia coronavirus.

Dunia ijikwamue na COVID-19 kwa uchumi sawia, wenye mnepo na unaojali mazingira:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Umoja wa Mataifa unataka dunia ifanye maamuzi ya kifedha ya kujikwamua kutoka kwenye janga la corona au COVID-19 ambayo yatazingatia athari za kijamii na kimazingira.

Akizungumza katika mkutano wa kundi jipya kutoka sekta binafsi kuhusu muungano wa uwekezaji wa kimataifa (GISD) kwa ajili ya maendeleo endeleo SDGs uliofanyika leo kwa njia ya mtandao , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Kujikwamua na kurejea katika hali ya ajira na uzalishaji katika viwango vya kabla ya janga hili itachukua muda, hivyo sekta binafsi zinahitaji kufanya maamuzi ya kifedha kwa kutilia maanani athari za kijamii na kimazingira.”

Katika Mkutano huo Guterres amelitaka kundi hilo la wawekezaji kusaidia kubadili janga la sasa kuwa fursa ya kujenga uchumi wa kimataifa ambao utakuwa wa usawa, unaojali mazingira na wenye mneo utakaojumuisha kila mtu.

Teknolojia

Kundi hilo la wawekezaji limewaleta pamoja takribani wakuu 30 wa taasisi za fedha. Makampuni na viwanda na watoa huduma za kiteknolojia.

Watu haw ani wamiliki, mameneja wasimamizi wa mali na makampuni kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

Katibu Mkuu amesema ushawishi na uzoefu wa kundi hili la biashara la kimataifa unaweza kusaidia kuongeza mchango wa sekta binafsi katika malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Pia ametaja athari mbaya za janga la COVID-19 kuwa ni “Pamoja na ongezeko la ukosefu wa ajira na kufungwa kwa muda biashara ambao sasa kunaonekana kuwa ni kwa moja kwa moja.” Akiongeza kuwa kujerea tena kwa ajira katika hali ya kabla ya janga la corona ni suala litakalochukua miaka mingi.

Malengo ya kimataifa

Umoja wa Mataifa umesema kuwa changamoto ya sasa ya kiuchumi inaziweka hatua zilizopigwa za maendeleo katika hatari kwa kuifanya dunia kwenda mrama katika hatua za ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu amesisitiza kwamba “Wakati wote watu masikini na walio hatarini ndio wanaoathirika Zaidi na kupoteza ajira na maradhi, kuelemewa na mzigo wa afya na mifumo duni na kukosa mfuko wa hifadhi ya jamii.”

Ametoa amekumbusha lengo la mwakilishi maalum kuhusu hatua za mabadiliko ya tabianchi na fedha , Mark Carney la kuhakikisha kwamba maamuzi yote ya masuala ya kifedha yanazingatia athari za kijamii na kimazingira.

Kwake lengo hilo ni muhimu zaidi katika miezi ijayo kuliko wakati mwingine wowote na kusema kwamba makampuni , wawekezaji nan chi lazima zifanye maamuzi makubwa ya kifedha kuhusu mustakbali wao.

Wanawake wakifanya kazi shambani katika Jimbo la Jubek, Sudani Kusini, ambapo WFP inakuza kilimo endelevu ili kuimarisha mapato na maisha.
WFP/Giulio d'Adamo
Wanawake wakifanya kazi shambani katika Jimbo la Jubek, Sudani Kusini, ambapo WFP inakuza kilimo endelevu ili kuimarisha mapato na maisha.

 

Kipindi cha mpito

Antonio Guterres ametoa wito wa kuchukuliwa hatua na jumuiya ya biashara , kwanza kuwasliana kwa mujibu wa kikozi kazi cha masuala ya ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi na kuunga mkono wito wa kufanya wajibu huu kutimia.

Pili wajibu ni kwa sekta binafsi kutathimini athari za hatari za mabadiliko ya tabianchi katika kuanzisha miundo ya biashara.

Na mwisho ametoa wito wa mipango ya mpito kuweza kufikia kutokuwa na hewa ukaa chafuzi kabisa katika makampuni yanayowakilishwa na GISD.

Kwa Guterres majanga kwa kawaida huwa ni mengi na makubwa na yanahitaji ongezeko la rasilimali ambazo tayari ni finy una kusababisha madhila makubwa kwa binadamu.

Hivyo ameomba kwamba janga la sasa litumike kuunda mustakabali bora.