Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti kuu ya kiuchumi yaangazia kwa nini ushirikiano wa kimataifa ni muhimu

Waachuuzi wakazi wa Kampala wakiwa sokoni nchini Uganda.
Arne Hoel/World Bank
Waachuuzi wakazi wa Kampala wakiwa sokoni nchini Uganda.

Ripoti kuu ya kiuchumi yaangazia kwa nini ushirikiano wa kimataifa ni muhimu

Ukuaji wa Kiuchumi

Ukuaji wa uchumi duniani unatarajiwa kupungua kutoka wastani wa asilimia 2.7 mwaka 2023 hadi asilimia 2.4 mwaka 2024, ukiwa chini ya kiwango cha ukuaji wa kabla ya janga la COVID - 19 la asilimia 3.0, kulingana na Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Hali ya Kiuchumi na Matarajio ya Dunia (WESP) 2024 iliyozinduliwa leo Januari 04 mjini New York.

Utabiri huu wa sasa unakuja kufuatia utendaji wa uchumi wa dunia unaozidi matarajio katika 2023. Hata hivyo, ukuaji wa mwaka jana wa nguvu zaidi kuliko ilivyotarajiwa ulifunika hatari za muda mfupi na udhaifu wa kimuundo.

Aidha ripoti hiyo, inaonesha kuwa ukuaji wa Pato la Taifa lenye nguvu zaidi kuliko ilivyotarajiwa mwaka jana baada ya kutoka katika janga la COVID-19 ulifunika hatari za muda mfupi na udhaifu wa kimuundo katika uchumi wa dunia.

Utafiti unaegemea viwango vya juu vya riba vinavyoendelea, kuongezeka kwa migogoro, biashara ya kimataifa iliyodorora, na kuongezeka kwa majanga ya tabianchi, ambayo yote yanaleta changamoto kubwa kwa ukuaji wa kimataifa.

Inaangazia kipindi kirefu cha masharti magumu ya mikopo na gharama kubwa zaidi za kukopa, ikiwasilisha upepo mkali kwa uchumi wa dunia uliojaa madeni na kuhitaji uwekezaji zaidi ili kufufua ukuaji, kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kuharakisha maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).