Viwanda vidogovidogo vyalaumiwa kuchafua vyanzo vya maji
Maji safi na salama ni uhai wa viumbe vyote ulimwenguni ikijumuisha binadamu, wanyama na mimea. Lengo namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu, SGD linazungumzia maji safi na salama kwa kila mtu ifikapo ya mwaka 2030.
Katika migogoro ya kimazingira, viwanda vidogo na vikubwa vimekuwa vikilalamikiwa kuharibu mazingira kwa kujenga mifereji inayopeleka maji taka katika vyanzo vya maji au mito.