Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nchi 90 zasisitiza ahadi yao ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa

Wawakilishi wanaunda nchi 91 wameeleza kujitolea kwao kwa pamoja kwa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa
Wawakilishi wanaunda nchi 91 wameeleza kujitolea kwao kwa pamoja kwa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya nchi 90 zasisitiza ahadi yao ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa

Amani na Usalama

Mkutano huu wa Mawaziri wa 2023 wa Mawaziri wa ulinzi uliofanyika jijini Accra, nchini Ghana uliokamilika leo jijini Accra, Ghana umepata ahadi mpya, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi na mafunzo, ili kukabiliana na changamoto na mahitaji ya sasa na ya baadaye ya ulinzi wa amani duniani.

Walinda amani wanahudumu katika mazingira magumu zaidi duniani na vitisho vinavyowakabili ni vikubwa zaidi kuliko hapo awali, na kuongezeka kwa mivutano ya kijiografia, migogoro migumu zaidi, na utumiaji silaha wa zana za kidijitali dhidi yao na jamii wanazohudumia.

Jean-Pierre Lacroix, Msaidizi wa Katibu Mkuu na mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa leo amehutubia mkutano huo, ambapo zaidi ya nchi 90 zimesisitiza ahadi yao ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa. 

Bwana Lacroix ameeleza kuwa lengo kuu la ulinzi wa amani ni kusaidia kutatua migogoro ili kupata na kutekeleza mikataba ya amani na michakato inayohusiana ya kisiasa. "Mafanikio yake, katika suala hili, katika historia yake ya miaka 75 haipaswi kusahaulika katika ukungu wa vita ambao unaendelea kuharibu mataifa na idadi ya watu iliyo dhaifu zaidi ulimwenguni. Lakini ulinzi wa amani sio fimbo ya uchawi na hauwezi kufanikiwa peke yake, kupata amani endelevu kunahitaji utashi wa kisiasa na ushiriki wa pamoja wa Nchi Wanachama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Ghana, Shirley Ayorkor Botchwey amesema kuwa jumla ya nchi 91 na mashirika matatu ya kimataifa yameelezea dhamira yao ya pamoja na uungaji mkono wa kisiasa wa ulinzi wa amani ikiwa ni mkutano wa hivi karibuni zaidi katika mfululizo wa mikutano iliyofanyika. 

Nchi wanachama 57 pia zimetangaza ahadi mpya za kujaza mapengo muhimu na kuimarisha ufanisi katika kutoa kazi zilizoamriwa, ikiwa ni pamoja na kuzuia ghasia, kulinda raia na kujenga amani. "Ahadi madhubuti zinazotokana na tukio hili la kihistoria zitatoa utoaji wa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa zinazohitaji kutekeleza majukumu magumu katika mazingira magumu,"

Kwa kumalizia, Waziri wa Ulinzi wa Ghana Dominic Nitiwul amesema uhusiano ulioanzishwa na ahadi zilizotolewa hazitakuwa za muda mfupi. "Ni mbegu zilizopandwa kwa ajili ya ulimwengu wenye amani na usalama zaidi, mavuno ambayo tutavuna katika miaka ijayo."

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Ulinzi wa Amani kwa ngazi ya mawaziri kufanyika katika bara la Afrika. Awali mkutano hii ilifanyika Marekani, Uingereza, Canada na Jamhuri ya Korea. Kongomano kama hili kwa mwaka wa 2025 litafanyika Ujerumani.