Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri kutoka nchi wachangiaji wa vikosi vya ulinzi wa amani wakutana UN

Wanawake siku zote wamekuwa na mchango na jukumu muhimu katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Wanawake 12 kutoka kikosi cha askari watembea kwa miguu walikuwa wanawake wa kwanza walinda amani kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa nchi
UN /John Isaac
Wanawake siku zote wamekuwa na mchango na jukumu muhimu katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Wanawake 12 kutoka kikosi cha askari watembea kwa miguu walikuwa wanawake wa kwanza walinda amani kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa nchi

Mawaziri kutoka nchi wachangiaji wa vikosi vya ulinzi wa amani wakutana UN

Amani na Usalama

Ujumbe wa watu 125 wakiwemo mawaziri zaidi ya 60 kutoka kote duniani wanakutana leo kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kwa ajili ya kutamini utendaji wa vikosi vyao katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa na mbinu za kuuboresha.

 

Mkutano huo unaobeba kaulimbiu “Ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ngazi ya mawaziri:uwezo wa askari, utendaji na ulinzi” ni wa kuthibitisha dhamira na ahadi ya nchi zao katika operesheni za Umoja wa Mataifa na pia kujadili mbinu mujarabu za kuimairisha utendaji wao na ulizi wa raia kwa miaka mijayo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mkutano wa mwaka huu unatoa fursa kwa wajumbe kwa pamoja kuandaa mkakati wa uwezo maalumu na wa lazima kwa ajili ya operesheni za sasa za ulinzi wa amani za umoja wa Mataifa kama inavyohitajika na waraka wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa , ikijikita zaidi na kuongeza jukumu la wanawake katika ulinzi wa amani.

Mkutano huu pia unatupia jicho juhudi zinazoendelea za kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani kupitia mkakati wa hatua wa Katibu mkuu ujulikanao kama (A4P) na mapendekezo na mikutano mingine ya ngazi ya juu iliyofanyika kati ya 2014 na 2017 New York, Paris, London na Vancouver.

Mawaziri katika mkutano huo pia wananaelezea hatua zilizopigwa katika ahadi zilizowekwa nan chi wanachama za kushirikiana majukumu ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa na kutiwa saini wakati wa mkutano wa A4P septemba 25 mwaka 2018.

Kwenye ufunguzi wa mkutano huo Katibu Mkuu atakabidhi pia tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya mchechemzi wa kijeshi wa masuala ya kijinsia kwa Kamanda Luteni Marcia Andrade Braga kutoka Brazil ambaye hivi sasa anahudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA.

Wengine wanaozungumza kwenye mkutano huo ni Angelina Jolie, mwanzilishi mwenza wa mradi wa kuzuia ukatili wa kingono katika mizozo (PSVI),na ambaye pia ni balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), akijikita katika wito wa umuhimu wa ulinzi wa raia na kuzitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongeza ushiriki wa wanawake katika operesheni za ulinzi wa amani.