Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 75 ya Tamko la Haki za Binadamu bado biashara ya binadamu inashamiri: Türk

Lori lililojaa wahamiaji ambao ni vijana likijiandaa kusafiri hadi Agadez.
© UNICEF/Juan Haro
Lori lililojaa wahamiaji ambao ni vijana likijiandaa kusafiri hadi Agadez.

Miaka 75 ya Tamko la Haki za Binadamu bado biashara ya binadamu inashamiri: Türk

Haki za binadamu

Wigo wa kimataifa wa biashara haramu ya binadamu unahitaji mikakati iliyoratibiwa na inayonyumbulika, amesema Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Haki za Kibanadamu, OHCHR, akihutubia mkutano wa Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu  huko Vienna nchini  Austria, akiongeza kuwa, “biashara haramu ya kibinadamu na unyanyasaji wa watu kwa lengo la kuongeza faida ni mojawapo ya uhalifu wa zamani na wa kutisha zaidi kote ulimwenguni.

 

Bwana Türk ametoa wito akisema, “Tunapoadhimisha miaka 75 ya Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu, ninakualika kuweka haki za binadamu katikati ya majadiliano yako kuhusu "mipaka katika biashara haramu ya binadamu", ambayo ni mada ya mkutano huu.” Na akuongeza kuwa katika karne ya 21, usafirishaji haramu wa watu umeendelea kustawi, hasa pale ambapo migogoro ya silaha, mdororo wa kiuchumi, dharura za kiafya, uhaba wa chakula, majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na majanga mengine ya kibinadamu yanazidisha ukatili uliopo. “Inakadiriwa kuwa hii ni shughuli haramu ya 3 yenye faida kubwa zaidi kote ulimwenguni kwa vile kila eneo limehusishwa na janga hili.”

Kulingana na takwimu za kimataifa za hivi karibuni, kuna watu milioni 49.6 wanaolazimishwa kufanya kazi au kuolewa kila uchao, asilimia 25 zaidi ukilinganisha na mwaka wa 2016. Hii ni miongoni mwa mamilioni ya wanaume, wanawake na watoto, walionyanyaswa katika lindi la ushirikina wa kingono, utumikishwaji wa lazima, ndoa za kulazimishwa, biashara ya dawa za kulevya, utumwa wa nyumbani, kuondolewa kwa viungo, na mambo mengine ya kutisha.

Wakimbizi na wahamiaji wanaokimbia mateso, vurugu au kutafuta maisha bora, wako hatarini haswa, sio tu katika nchi zao za asili, bali pia katika nchi zinazowapokea kama wakimbizi.

Wanawake na wasichana wameathirika kwa njia isiyo sawa, inayowakilisha zaidi ya asilimia 70 ya waathiriwa wote waliogunduliwa kote ulimwenguni. Wanasafirishwa kwa wingi kwa ajili ya ukatili wa kingono na ndoa za kulazimishwa; ambapo wanaume na wavulana wanajumuishwa kuwa sehemu kubwa zaidi ya waathiriwa waliogunduliwa wa kusafirishwa kwa ajili ya kazi za kulazimishwa.

Watoto ni theluthi moja ya waathiriwa wote waliogunduliwa.

Bwana Turk amepongeza Kikosi Kazi cha Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu cha Austria kwa kuitisha mkutano huu wa kila mwaka kuhusu suala ambalo ni tata sana, linalohitaji majibu kurekebishwa na kuratibiwa mara kwa mara. Isitoshe, aina za unyonyaji na mbinu zinazotumiwa na wahalifu zinaendelea kudorora. Teknolojia ya kisasa ya soko la usafirishaji haramu la watu katika muongo mmoja uliopita, huku mitandao ya kijamii na programu zao mitandao Pamoja na tovuti za Intaneti zilitumika kuajiri, kutangaza na kuuza waathiriwa, wengi wao wakiwa watoto.

“Hali ya kimataifa ya usafirishaji haramu wa binadamu pia hufanya ushirikiano na ubia kuwa muhimu.” Ameongeza Bwana Turk akitolea mfano Ofisi yake kwamba ni mwanachama wa Kikundi cha Uratibu wa Mashirika ya Kimataifa dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu, kinachofanya kazi kwa pamoja na mashirika mengine 27 ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa na kusisitiza kuwa ushirikiano wa karibu unahitajika kati ya Mataifa, mashirika ya kimataifa na kikanda, watendaji wa kijamii, mashirika ya kiraia, na sekta binafsi miongoni mwa wengine.

Usafirishaji haramu wa binadamu, bila shaka, ni suala kubwa la haki za binadamu, ukiukaji na unyanyasaji unaofanywa dhidi ya waathiriwa, lakini wale ambao tayari wanaishi katika mazingira magumu zaidi wako hatarini pia. Mbinu inayozingatia haki za binadamu inatoa mfumo wa kuzuia na kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu, ambao unawaweka watu katikati.

Hii inamaanisha kushughulikia sababu za msingi za usafirishaji haramu wa binadamu ili kuzuia uhalifu huu kutokea mara ya kwanza. Hii ni pamoja na hatua za kupunguza mahitaji ya usafirishaji haramu wa binadamu kama sehemu ya minyororo ya thamani ya kimataifa, kwa kudhibiti mwenendo wa biashara na kujumuisha uzingatiaji wa haki za binadamu katika michakato ya ununuzi.

Vile vile inamaanisha kuhakikisha usaidizi, ulinzi, na upatikanaji wa haki na masuluhisho kwa waathiriwa, bila kujali hali ya makazi, uwezo au nia ya kushirikiana na mashirika ya haki ya jinai, au utambuzi, uchunguzi na mashtaka ya wahalifu. Kuimarisha uwezo wa utambuzi wa mapema wa wahasiriwa, pamoja na polisi, wakaguzi wa kazi na maafisa wa uhamiaji, ni muhimu. Kwa mfano, Ofisi yangu, kwa pamoja na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga, ICAO, imeandaa miongozo kwa waendeshaji wa mashirika ya ndege ili kuwafunza wafanyakazi wa kambi katika kutambua na kuripoti watu wanaosafirishwa.

Mtazamo unaozingatia haki za binadamu pia unamaanisha mikakati na huduma za kukabiliana na biashara haramu ambayo inahusisha ushiriki hai na mzuri wa waathiriwa na waathirika, kwa kuzingatia umri, jinsia na utofauti zao. Inamaanisha kuwa watu wanaosafirishwa haramu hawaadhibiwi kwa mwenendo usio halali ambao walifanya kama matokeo ya moja kwa moja ya kusafirishwa.

Amehitimisha kwa kusema, “Nyuma ya takwimu za unyanyapa kwa binadamu ni wanawake, wanaume na watoto wanaohitaji msaada wetu, na ambao wana haki ya maisha ya utu, uhuru na haki. Ninawasihi muweke masilahi yao mbele, na mtarajie kusikia matokeo ya mijadala yenu.”