Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti kuhusu kutokuwepo ubaguzi wa rangi wa kitaasisi Uingereza ni upotoshaji: Wataalam 

Watu wakiandamana mjini London kuunga mkono kampeni ya Black Lives Matter ambayo inapigania haki ya maisha ya mtu mweusi. Juni 2020.
Unsplash/James Eades
Watu wakiandamana mjini London kuunga mkono kampeni ya Black Lives Matter ambayo inapigania haki ya maisha ya mtu mweusi. Juni 2020.

Ripoti kuhusu kutokuwepo ubaguzi wa rangi wa kitaasisi Uingereza ni upotoshaji: Wataalam 

Haki za binadamu

Wataalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali ripoti inayoungwa mkono na serikali ya Uingereza kuhusu ubaguzi wakisema kwamba inapotosha zaidi na kuharamisha ukweli wa kihistoria kuhusu ubaguzi na kwamba inaweza kuchochea zaidi ubaguzi na ubaguzi wa rangi.  

Katika taarifa yao wataalam wa kikosi kazi cha wataalam hao kuhusu watu wenye asili ya Kiafrika wamesema  "Katika mwaka wa 2021, inashangaza kusoma ripoti kuhusu ubaguzi wa rangi na ukabila ambayo inarejesha tena alama za ubaguzi na ubaguzi  wa rangi kuwa ukweli, ikipotosha takwimu na kutumia vibaya takwimu hizo na utafiti katika matokeo na mashambulizi kwa watu wa asili ya Kiafrika.”  

Ripoti hiyo iliwasilishwa Machi 31 na tume kuhusu mapengo ya ubaguzi na ukabila iliyoundwa na serikali ya Uingereza baada maandamano makubwa yaliyozuka mwaka jana duniani ya Black Lives Matter na wataalam hao wanasema ripoti hiyo kimsingi inakataa kuwepo kwa ubaguzi wa rangi nchini Uingereza.  

Wataalam hao wa haki za binadamu pia wamesema kwamba ripoti hiyo ilinukuu "ushahidi wa kutia shaka kutoa madai ambayo yanatukuza wazungu kwa kutumia hoja zilizozoeleka ambazo kila wakati zimehalalisha ubaguzi wa rangi. 

"Jaribio hili la kuhalalisha ukuu wa wazungu licha ya utafiti mwingi na ushahidi wa ubaguzi wa rangi wa kimkakati ni upunguzaji mbaya wa fursa ya kutambua ukatili  na uhalifu wa zamani na michango ya wote kwa lengo la kusonga mbele." 

Wataalam hao wameitaka serikali ya Uingereza kukataa kimsingi matokeo ya ripoti hiyo na kuhakikisha kwamba "uhalisi sahihi wa ukweli wa kihistoria" kwani unahusiana na zahma za zamani na ukatili, haswa utumwa, na biashara ya utumwa wa Waafrika na ukoloni. 

Jaribio la kutosikia 

Kikosi Kazi hicho pia kimesema kwamba ripoti ya tume ya Uingereza iliondoa kipengele cha utambuzi wowote au uchambuzi wa ubaguzi wa kitaasisi ulioainishwa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu, pamoja na ukaguzi wa kikosi kazi cha 2012, uchunguzi wa hitiomisho wa Kamati ya Kutokomeza ubaguzi wa mauaji ya kimbari, na ripoti ya 2018 ya mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu aina za kisasa za ubaguzi wa rangi. 

Wataalam hao pia wamelaani madai ya ripoti hiyo kwamba wakati kuna uwezekano wa kuwa na vitendo vya ubaguzi wa wazi nchini Uingereza, inadai hakukuwa na ubaguzi wa kitaasisi. 

"Hitimisho la ripoti kwamba ubaguzi wa rangi ama ni tokeo la mawazo ya watu wa asili ya Kiafrika au ya tofauti, matukio ya binafsi linapuuza jukumu lililotapakaa wazi ambalo msingi wake ndio uliolewa ubaguzi katika jamii, haswa katika kuhalalisha ukatili, ambapo serikali ya Uingereza na taasisi zake zilikuwa na jukumu muhimu. ” 

Wataalam walibaini kuwa wakati tofauti za rangi zinaweza kuwa sio kila wakati zinatokana na ubaguzi au ubaguzi wa rangi, kuna ushahidi wa kushawishi kwamba mizizi ya tofauti hizi iko katika ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kimuundo, kwani hauonyeshi upendeleo au vipaumbele vya jamii zinazokabiliwa na ubasguzi wa muundo huo.  

"Maoni kwamba muundo wa familia, badala ya mazoea ya kibaguzi na ya kimuundo ni sifa kuu za uzoefu wa watu Weusi ni jaribio la kukataa hali halisi inayowakabili watu wa asili ya Kiafrika na makabila mengine nchini Uingereza", wamesisitiza wataalam hao.” 

Inasikitisha lakini sio jambo jipya 

Kikosi kazi pia kimesema kwamba ripoti hiyo ya uwakilishi potofu wa hadithi za utumwa ilikuwa ni jaribio la kusafisha historia ya biashara hiyo ya utumwa kwa Waafrika. 

"Hii ni mbinu mbaya, ingawa sio mbinu isiyo ya kawaida, iliyotumiwa na wengi ambao utajiri wao ulitokana moja kwa moja kwa kuwafanya watu wengine  watumwa wao, tangu utumwa ulipopigwa marufuku. Kutafuta kunyamazisha jukumu la kikatili la watumwa, utajiri wa kizazi uliotokana na utumwa na kijamii na ushawishi wa kisiasa waliopata kutokana na kutumia miili ya watu weusi katika biashara ya utumwa ni jaribio la makusudi la upotoshaji wa kihistoria. "