usafirishaji haramu wa binadamu

30 SEPTEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anamulika:

Taarifa ya kwamba hatua za kutokomeza ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika zinatekelezwa vipande vipande licha ya harakati zinazoendelea za kuondokana na ubaguzi wa kimfumo.

Nchini Ureno ,shirika moja lililoanzishwa na Maria Ramires linasaidia wanawake wazee kujijengea mnepo hata wakati wa utu uzima, mathalani kujifunza kuendesha merikebu zenye matanga.

Sauti
10'39"
Picha ya UNICEF/Alessio Romenzi

UNHCR yataka usaidizi zaidi wa ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji

Pengo la huduma za ulinzi safari latumbukiza wakimbizi mikononi mwa wasafirishaji haramu

Kuelekea sikuya kimataifa dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu kesoh Julai 30, shirika la umoja wa Mataifa la wakimbizi duniani, UNHCR imesema ukosefu wa huduma za ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji wanaofanya safari hatarishi kutoka ukanda wa Sahel na Pembe ya Afrika kwenda Afrika Kaskazini na kisha Ulaya, kunawatumbukiza katika hatari ya mikono ya wasafirishaji haramu. Leah Mushi na taarifa zaidi.

Sauti
2'23"

Julai 29, 2021

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepatia mafunzo ya mbinu za medani 

Nchi ya Bhutan yafanikiwa kutoa chanjo kwa 90% ya watu wake wanaotakiwa kupata chanjo

Pia utasikia makala ya binti mdogo manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu aliyesafirisha bila ridhaa yake na kubakwa.

Sauti
12'23"
UN

Watu wasafirishwa kiharamu ili kutumikishwa kwenye kuombaomba

Idadi ya watoto wanaosafirishwa kiharamu imeongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, huku idadi ya wavulana kwenye kundi hilo ikiwa imeongezeka mara 5, imesema ripoti mpya ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kukabili uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

Ripoti hiyo ya usafirishaji haramu wa binadamu duniani yam waka 2020  imezinduliwa mjini Vienna, Austria ikifafanua zaidi kuwa watoto wa kike wanasafirishwa kiharamu kwa ajili ya kutumikishwa kingono ilihali wavulana kutumikishwa kwenye ajira.

Sauti
3'8"