Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali katika Ukanda wa Gaza:UNRWA

Jengo moja likiwa linateketea kwa moto katikati mwa Gaza.
UN News/Ziad Taleb
Jengo moja likiwa linateketea kwa moto katikati mwa Gaza.

Hali katika Ukanda wa Gaza:UNRWA

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa kwakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema hali katika Ukanda wa Gaza ni tete huku maelfu ya watu wakiendelea kutawanywa na kusaka hifadi katika vituo vya shirika hilo.

Kwa mujibu wa tarifa ya shirika hilo iliyotolewa jioni ya leo mpaka wakati huu 

• UNRWA inawapa hifadhi wakimbizi wa ndani 73,538 (IDPs) katika shule zake 64 katika maeneo yote ya Ukanda wa Gaza. Kati ya hizo, shule 45 ni makazi teule ya dharura (DES) na 19 ya kawaida.

• Shule ya UNRWA inayohifadhi familia zilizohamishwa katika Ukanda wa Gaza imeathirika moja kwa moja. Shule hiyo inayohifadhi watu zaidi ya 225 imeharibiwa vibaya. Hakuna waliopoteza maisha walioorodheshwa miongoni mwa watu waliotawanywa shule imepata uharibifu mkubwa wa majengo yake.

Ulinzi kwa raia

• Wizara ya afya huko Gaza imeripoti kuuawa 370, ikiwa ni pamoja na angalau watoto 20, na wengine 2,200 kujeruhiwa tangu 7 Oktoba. Wanafunzi watatu wa UNRWA katika shule za UNRWA huko Khan Younis na Beit Hanoun, wote wavulana, wamethibitishwa kuuawa.

• Kulingana na vyanzo vya wazi vya Israeli, watu zaidi ya 650 wameuawa nchini Israeli.

Katikati ya Gaza kumeripotiwa kushambuliwa
UN News/Ziad Taleb
Katikati ya Gaza kumeripotiwa kushambuliwa

Kuhusu elimu

Kuhusu suala la elimu UNRWA inasema 

• Shule zote za UNRWA katika Ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kituo cha mafunzo kwa wenye ulemavu wa macho na vituo viwili vya ufundi huko Gaza na Khan Younis, vimefungwa. 

• Zaidi ya wanafunzi 300,000 wameathirika na hali hii

Utoaji wa huduma za afya

• Vituo vya afya 15 kati ya 22 vya UNRWA kote Ukanda wa Gaza vimeanza tena kutoa huduma za afya ya msingi kuanzia saa tatu asubuhi  hadi saa sita mchana kwa wagonjwa waliopewa miadi ya haraka iliyopokelewa kupitia nambari ya simu ya bure (1-800-444). -666) NB1

• Vituo vya Afya vinatoa matibabu kwa magonjwa yasiyoambukiza na kwa wagonjwa muhimu wa nje.

• Hadi asilimia 13 ya jumla ya wafanyakazi wa huduma za afya wa UNRWA wapo.

• Utoaji wa huduma za afya ya dharura kupitia simu ya bure  nambari 1-800-444-666 unaendelea katika maeneo yote. Takriban simu 1,500 zimepokelewa kwenye simu hiyo isiyolipishwa na UNRWA imetoa huduma husika.

Hali ya uharibifu katikati ya Gaza
UN News/Ziad Taleb
Hali ya uharibifu katikati ya Gaza

Utoaji wa Huduma za usafi wa mazingira

• Operasheni za ukusanyaji na uhamishaji wa taka ngumu kwenye dampo zinasalia kusitishwa.

• Uendeshaji wa visima vya maji huko Jabalia, Khan Younis na Rafah unaendelea.

• Timu ya matengenezo ya UNRWA imefanya kazi za matengenezo ya pampu ya maji ili kutoa maji katika shule ya Rafah prep boys B, ambayo ni makazi teule ya dharura.

Msaada na huduma za kijamii

• Operesheni za chakula zinasalia kusitishwa hadi taarifa zaidi zitakapopatikana na hivyo kutatiza mzunguko wa tatu wa usambazaji wa chakula. Vituo 14 vya usambazaji wa vyakula vimefungwa. Takribani familia 112,759  sawa na watu 541,640 bado hawajapokea msaada wa chakula

• Nambari za simu za msaada na huduma za kijamii zinafanya kazi na zimepokea simu 27 kuanzia saa nane mchana leo. Haya yalikuwa maombi mengi ya habari kuhusiana na msaada wa chakula, huduma tembezi za dawa na msaada wa makazi.

• Msaada wa kisaikolojia na msaada wa huduma ya kwanza wa kisaikolojia umetolewa kwa njia ya simu kwa karibu watu 80.

• Theluthi mbili ya wafanyakazi wa huduma za jamii wanatoa huduma kwa mbali, ikijumuisha msaada wa uingiliaji kati wa kijamii, ushauri wa kisheria na huduma za simu.

• Huduma za usajili pia zinapatikana.

Wanaume wakitembea katika eneo lilosambaratishwa vibaya katikati ya Gaza
UN News/Ziad Taleb
Wanaume wakitembea katika eneo lilosambaratishwa vibaya katikati ya Gaza

Operesheni za jumla za UNRWA

• Hali ya wafanyakazi wa UNRWA kutokja sehemu moja Kwenda nyingine imebakia kuwa na vikwazo isipokuwa kwa wafanyakazi wanaotoa huduma.

• Mafuta yalisambazwa kwa vituo vya afya vya UNRWA.

• UNRWA inashiriki taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwa jamii zilizoathirika kuhusu huduma za afya zinazopatikana katika vituo 15 vya afya.

• Angalau mitambo 14 ya UNRWA ilipata uharibifu katika siku chache zilizopita.