Mkurugenzi Mkuu wa IAEA aonya kuhusu hofu ya kutokuwa na uwazi wa nyuklia Iran na kusisitiza diplomasia
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Mariano Grossi, amewasilisha taarifa kali kwa Bodi ya Magavana ya shirika hilo leo, akieleza wasiwasi mkubwa kuhusu kushindwa kwa Iran kushirikiana ipasavyo na wakaguzi wa nyuklia.
Hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi vyaliacha hoi bara la Afrika yaonya WMO.
Ripoti mpya kuhusu “Hali ya Hewa Afrika 2024” iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO imeonya kwamba muongo wa joto zaidi kuwahi kushuhudiwa Afrika umeleta madhara makubwa kwa bara hilo. Evarist Mapesa na taarifa zaidi
Vita Sudan yamsababishia Walaa tatizo la afya ya akili
Tarehe 15 mwezi April imwaka 2023 wananchi wa Sudan hususan mji mkuu Khartoum waliamshwa na mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa kikosi cha msaada wa haraka RSF. Hadi leo hii mapigano hayo yanazidi kushika kasi na raia wanafurushwa makwao. Miongoni mwao ni watoto ambao zahma wanayokutana nayo sio tu kufurushwa bali pia changamoto ya afya ya akili. Tayari shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limeona shida hiyo na limeanza kuchukua hatua kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.
Fahamu mambo 5 muhimu kutoka hotuba ya Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini kwa UNGA78
Afrika haiko tayari kuendelea kubeba gharama za mapinduzi ya viwanda na maendeleo ya nchi tajiri, ni moja ya kauli kutoka hotuba ya Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akihutubia mjadala mkuu wa UNGA78 jijini New York, Marekani.
Afrika fikiria upya kupanua wigo wa bidhaa za kuuza nje- UNCTAD
Hii leo ikiwa ni siku ya Afrika, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD imesema siri ya kujikwamua kwa bara hilo kiuchumi ni kupanua wito wa bidhaa inazouza nje.