Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Apu ya OKY na hedhi salama yasongesha SDG 3- UNICEF

Wasichana wa baraza la ushauri la vijana, Nairobi wakitazama app ya OKY.
UNICEF Kenya
Wasichana wa baraza la ushauri la vijana, Nairobi wakitazama app ya OKY.

Apu ya OKY na hedhi salama yasongesha SDG 3- UNICEF

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limezindua apu maalum ya wasichana kufuatilia maelezo wakati wa hedhi. Apu hiyo ni mahsusi kwa wasichana wa mataifa yanayoinukia na yaliyo masikini. Apu hii inaleta matumaini wakati huu ambapo viongozi wa dunia wanakutana New York, Marekani kutathmini maendeleo ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. 

UNICEF iko mstari wa mbele kutoa maelezo kuhusu hedhi kwa wasichana wa Kenya. Agnes Makanyi ni afisa wa usafi na masuala ya hedhi wa UNICEF na anaeleza kuwa Dhamira ni kuwaelimisha wasichana kwani, “UNICEF inataka kuhakikisha wasichana wako ndani ya dijitali ama kutumia vifaa vya dijitali, simu za mkononi ndio waweze kupata maelezo ya hedhi.Pia wanaweza kufuatilia mzunguko wa hedhi hata walio na ulemavu pia wanaweza kuitumia . 

Apu ni bure kupakua na kuitumia 

Kwa ushirikiano na shirika la kijamii la LVCT Health, wasichana wa shule wanaweza kupata maelezo ya jinsi ya kufuatilia mzunguko wa hedhi kila mwezi. Mercy Nzuki ni afisa wa mradi kutoka LVCT Health na anafafanua kuwa ni rahisi kwa msichana kutumia Apu ya OkY kwani,Kwa kupakua msichana anahitaji mtandao lakini baada ya hapo anaweza kuitumia bila intaneti.Uzuri wa Apu hii ni ya bure.Haitozi ada yoyote.” 

Kwa UNICEF, dhamira ni kuondoa hali ya kutojua na kuelewa masuala ya hedhi na jinsi ya kujitazama katika kipindi hicho. Hii ni kwasababu baadhi ya wasichana hawana pa kukimbilia kupata maelezo sahihi. Agnes Makanyi ni afisa wa usafi na masuala ya hedhi wa UNICEF na anasisitiza kuwa ni rahisi kupata maelezo kwenye Apu ya OKY ambapo, “mchango wa UNICEF katika uzinduzi wa matumizi ya hii Apu ni kuhakikisha kila msichana katika Kenya ameweza kuipakua ili apate maelezo ya wakati wa hedhi.Pia UNICEF inahakikisha kwamba wasichana wanapata huduma bora za maji na usafi kupitia vyoo salama na pia kunawa mikono kwa maji na sabuni.” 

Merci Niybeshaho (wa pili kushoto), Rais wa Baraza la ushauri wa vijana, Nairobi (kushoto) Irene Wangui, mwanachama wa baraza la ushauri la vijana Nairobi.
UNICEF Kenya
Merci Niybeshaho (wa pili kushoto), Rais wa Baraza la ushauri wa vijana, Nairobi (kushoto) Irene Wangui, mwanachama wa baraza la ushauri la vijana Nairobi.

Apu ya OKY haina matangazo ya biashara 

Ili kuwafikia wasichana wengi zaidi, Apu ya OKY inaweza kutumika bila mtandao baada ya kuipakua. Kadhalika inatuma nafasi kidogo kuihifadhi kwenye simu ya mkononi na sio lazma iwe ya ghali. Apu ya OKY inaweza kutumiwa na programu ambazo sio mpya bila malipo na haina matangazo ya biashara. 

Kwa sasa apu ya OKY  iko kwenye Android pekee 

Apu ya OKY inafanya kazi kwenye simu aina ya Android na unaweza kuipakua kupitia Googleplay kwa lugha za kiingereza na kiswahili. Mtumiaji anaweza kufuatilia mzunguko wake wa hedhi Pamoja na kuweka kalenda na kupata maelezo. Maelezo yaliyomo yanauongeza uwezekano wa kupata yale ya sahihi kama anavyoelezea Irene Wangui, mwanachama wa baraza la vijana kutoka kaunti ya Nairobi na anasema ame ameona inawasaidia sana, “tunafahamishwa kuhusu njia bora za kujitazama na kudumisha usafi wakati wa hedhi.Apu inavutia na inampa mtumiaji motisha kuitumia.Pia ina shajara, unaweza kuhifadhi kumbukumbu na kujipanga...kwa mfano hisia zako.Nilihisi ina mengi na inanileta karibu na suala zima.Ningependa emoji ziongezwe.” 

Apu inatumia lugha za kiingereza na kiswahili 

Wasichana wanaoishi vijijini au mitaa ya mabanda hutatizika katika kipindi cha hedhi ukizingatia kupata maji safi na kudumisha afya. Hilo linachangia kwa wasichana kutoenda shule kwa hofu au kukosa bidhaa za usafi kama vile sodo.  

OKY Apu inawasaidia wasichana wa Ma daraja yoyote ya elimu kupata maelezo na hata walio na changamoto za kuona pia wanapata kuyasikiliza bila kutazama.  

Mary Anne Wanjiru Wambugu ni afisa wa masuala ya vijana katika serikali ya Kaunti ya Nairobi na Ana imani kuwa Apu ya OKY ni mwokozi kwavile, “Apu ya OKY inavutia sana. Sasa tuna mahali pa kukimbilia… Palipo na maelezo sahihi… ili Tuweze kupitisha maamuzi yanayofaa maishani. Unaweza kuwa na akaunti kadhaa kutumiwa na dada na marafiki. Tunaweza kusambaziana maelezo na Kubashiri lini hedhi zitaonekana. 

Apu kusambazwa pia Burundi, Afrika Kusini na Tanzania 

Mipango inaendelea kuwezesha Apu ya OKY kutumika kwa urahisi katika mataifa ya Burundi, Afrika Kusini na Tanzania. Lengo ni kuwa na jamii ya wasichana walioelimika ili kuwa na maisha bora zaidi. Hatua Hii inachangia katika kutimiza malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa, SDG ya elimu na afya. 

 

TAARIFA HII IMEANDALIWA NA THELMA MWADZAYA UN NEWS NAIROBI, KENYA