Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la kigaidi huko Baghdad mwaka 2003 limechukua sehemu ya Uhai wangu

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad, yaliharibiwa na bomu mnamo Agosti 19, 2003.
UN Photo/Timothy Sopp
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad, yaliharibiwa na bomu mnamo Agosti 19, 2003.

Shambulio la kigaidi huko Baghdad mwaka 2003 limechukua sehemu ya Uhai wangu

Amani na Usalama

Mjane wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambaye alikufa katika shambulio la kigaidi kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad, Iraqi amekuwa akielezea jinsi “tukio hilo lililogharimu maisha ya mume wake “lilivyochukua semehu ya Uhai wake.” 

Mume wa Laura Dolci, marehemu Jean-Selim Kanaan, alikuwa ametumwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Miradi kufanya kazi kama Msaidizi Maalum wa Mkuu wa Wafanyakazi wa Misheni ya inayohusika na Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq.

Ikiwa ni miaka 20 baada ya shambulio hilo na dunia ikiadhimisha Siku ya Ubinadamu Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Agosti, Laura anamkumbuka mumewe.

"Katika shambulio la kigaidi dhidi ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad mnamo 19 Agosti 2003, nilimpoteza Jean-Selim Kanaan, mume wangu wa miaka 33 na baba wa mtoto wetu mchanga.

Tulikutana Bosnia, kisha tukahamia pamoja Kosovo na baadaye New York, tukiwa na upendo mkubwa na tulikuwa tunadumisha maadili na upendo uleule kwa bendera ya buluu (akimaanisha Umoja wa Mataifa). Ama hakika kifo chake kimechukua kipande cha maisha yangu. 

Laura Dolci na marehemu mume wake, Jean-Selim Kanaan.
© Laura Dolci
Laura Dolci na marehemu mume wake, Jean-Selim Kanaan.

Laura anasema alipoamua kuendelea kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa lilikuwa chaguo gumu kwake, lakini chaguo ambalo limemsaidia kujua maana na sababu ya maisha yake na jinsi ya kupona kutokana na kitendo hicho cha kihalifu cha kutisha. “Kwa sasa mimi ni Katibu wa Mapitio ya Mara kwa Mara ya Baraza la Haki za Kibinadamu.”

Tarehe 19 Agosti imechorwa katika kila seli za mwili wangu. Ni sehemu yangu na maisha ya familia yetu. Ina maana mtoto wetu aliyekua bila kumjua baba yake. Bomu hilo la tani mbili lililemaza familia yetu kikatili, lakini tulishikiliana pamoja, tukihamasishwa na Jean-Selim, na tukaendelea, tukitoa maana kwa uwepo wetu na kushikilia juu tunu za ubinadamu na haki, nyumbani na kazini.

Shambulio hilo na muitikio wa Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa dunia ni tata, huku vitisho vipya vikiibuka.

Walakini, hii ni taaluma kubwa, na ninafurahi kuona kwamba urithi wa Sérgio Vieira de Mello, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ambaye pia alikufa katika shambulio hilo. Yeye na wenzake wanaendelea kuhamasisha kizazi kipya cha watumishi wa umma wa Umoja wa Mataifa.

Ninatumai, hata hivyo, kwamba maadhimisho haya ya ishirini ya siku ya Ubinadamu duniani pia yatakuwa hafla kwa familia ya UN kutafakari juu ya jinsi bora ya kufanya kazi katika hali ngumu za sasa.

Natumai bendera ya Umoja wa Mataifa itapata mwanga wake tena. Tunahitaji Umoja wa Mataifa wenye nguvu zaidi, unaojadili amani, upatanishi ili kuzuia na kukomesha migogoro.

Wenzetu waliotangulia mbele za haki wangetaka hilo.