Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UN lalaani shambulio la kigaidi nchini Afghanistan

Baraza la Usalama likijadili hali ya usalama nchini Afghanistan (Maktaba)
UN Photo/Eskinder Debebe
Baraza la Usalama likijadili hali ya usalama nchini Afghanistan (Maktaba)

Baraza la Usalama la UN lalaani shambulio la kigaidi nchini Afghanistan

Amani na Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la kigaidi dhidi ya Ubalozi wa Pakistan ulioko Kabul nchini Afghanistan, tarehe 2 Desemba 2022, ambapo Mkuu wa Mabalozi alishambuliwa na mlinzi wake kujeruhiwa vibaya.

Taarifa iliyotolewa hii leo kutoka jijini New York Marekani imesema wajumbe hao wa wamewatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Taarifa hiyo imeelewa wajumbe wa Baraza hilo la Usalama wametoa wito kwa pande zote husika kuheshimu na kuhakikisha kuna ulinzi na usalama wa majengo ya kidiplomasia na kibalozi na wafanyakazi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Pia wamesisitiza kutokiuka kanuni ya msingi kwa majengo ya kidiplomasia na kibalozi, na majukumu ya kupokea Mataifa, chini ya Mkataba wa Vienna wa Mahusiano ya Kidiplomasia wa mwaka 1961 na Mkataba wa Vienna wa mwaka 1963 wa Mahusiano ya Kibalozi.

Wametaka kuchukuliwe hatua zote zinazofaa kulinda kidiplomasia na majengo ya kibalozi dhidi ya uvamizi au uharibifu wowote na kuzuia uvunjifu wowote wa amani wa misheni hizi au uharibifu wa utu wao na shambulio lolote kwenye majengo ya kidiplomasia, mawakala na maafisa wa kibalozi.

Wajumbe wa Baraza la Usalama walisisitiza haja ya kuwawajibisha wahalifu, waandaaji, wafadhili na wafadhili wote wa vitendo hivi vya ugaidi na kuwafikisha mbele ya sheria.

Wamehitimisha taarifa yao kwa kuhimiza mataifa yote, kuzingatia wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa na maazimio husika ya Baraza la Usalama, kushirikiana kikamilifu na mamlaka zote husika.