Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zinazo zozana nchini Ethiopia zatakiwa kumaliza tofauti zao ili kulinda amani

Mgogoro wa kaskazini mwa Ethiopia umesababisha mamilioni ya watu kuhitaji msaada wa dharura na ulinzi.
© UNICEF/Christine Nesbitt
Mgogoro wa kaskazini mwa Ethiopia umesababisha mamilioni ya watu kuhitaji msaada wa dharura na ulinzi.

Pande zinazo zozana nchini Ethiopia zatakiwa kumaliza tofauti zao ili kulinda amani

Amani na Usalama

Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu kuhusu Ethiopia imeeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama inayoripotiwa kuzorota katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Ethiopia, hasa huko Amhara.

Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi imesema tume hiyo imezitaka pande zinazo zozana nchini humo kuheshimu haki za binadamu na kuchukua hatua za kupunguza hali hiyo na kuweka kipaumbele katika mchakato wa kutatua tofauti zao kwa amani.

Taarifa hii inakuja kufuatia tangazo lililo tolewa nchini Ethiopia tarehe 4 Agosti 2023 la Baraza la Mawaziri huwa nchi ipo katika hali ya hatari kwa Tangazo Na. 6/2023, ambalo chini ya Katiba linahitaji idhini ya bunge.

Matangazo ya Hali za hatari yaliyotangulia yamekuwa yakiambatana na ukiukwaji wa haki za binadamu, na hivyo Tume inaitaka Serikali ya Ethiopia kuzingatia kikamilifu kanuni za ulazima, uwiano na kutombagua mtu kwa mujibu wa wajibu wa nchi hiyo wa sheria ya kimataifa chini ya Ibara ya 4 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa.

Jukumu la Tume nchini Ethiopia

Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 17 Desemba 2021 liliiagiza Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu nchini Ethiopia kufanya uchunguzi wa kina na usiopendelea upande wowote kuhusu tuhuma za uvunjifu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa za haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu na sheria ya kimataifa ya wakimbizi nchini Ethiopia tangu tarehe 3 Novemba 2020.

Kupitia azimio la Baraza la Haki za Kibinadamu A/HRC/RES/51/27 wakati wa Kikao cha 51 cha Baraza hilo jijini Geneva Uswisi, Mamlaka ya Tume hiyo ya Ethiopia yaliongezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi kufikia mwezi Desemba 2023.