Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu mashuhuri 6 wajumuishwa kwenye jopo la wachechemuzi wa SDGs

Wachechemuzi wa malengo endelevu, SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 2015
UN SDGs
Wachechemuzi wa malengo endelevu, SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 2015

Watu mashuhuri 6 wajumuishwa kwenye jopo la wachechemuzi wa SDGs

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Wakati Umoja wa  Mataifa na wadau wake duniani kote wanahaha kusongesha na kufanisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030, wajumbe wengine wapya 6 wenye ushawishi wamejumuishwa kwenye bodi ya watetezi wa SDGs hii leo na kuahidi kusongesha malengo hayo kwa niaba ya amani, ustawi, wakazi wa Dunia na ubia.

“Tunazo mbinu za kujibu hoja zitokanzo na changamoto kama vile mabadiliko ya tabianchi, shinikizo kwenye mazingira, umaskini na ukosefu wa usawa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitangaza jopo hilo hii leo Alhamisi

Guterres ameongeza kuwa  “mbinu zimejikita kwenye makubaliano makubwa yam waka 2015 yaani ajenda ya 2030 ya maendeleo endeleuvu na mkataba wa Paris wa mabadilko ya tabianchi.”

Hata hivyo Katibu Mkuu amesema mbinu hizo hazina maana iwapo hazitatumika kwa hiyo “hii leo na kila siku ujumbe wangu ni rahisi. Tunahitaji kuchukua hatua, kuwa na malengo ya juu na utashi wa kisiasa. Hatua zaidi zahitajika na utashi zaidi wa kisiasa,” amesema.

Wajumbe hao 6 wapya wanaungana na wengine 11 na hivyo kuwa na kundi la watu mashuhuri 17 ambao wamejitolea kuhamasisha na kuchochea na kusongesha haraka hatua kwa kufanikisha SDGs ambazo ni pamoja na kutokomeza njaa, umaskini na huduma ya afya bora kwa wote.

Wachechemuzi hao wa SDGs wanajumuisha taswira nzima ya SDGs wakitoka serikalini, sekta ya burudani, wanazuoni, michezo, biashara na wanaharakati.

Mwenyekiti mwenza wa jopo hilo la watu 17 Waziri Mkuu Erna Solberg wa Norway amesema “kwa kuunganisha nguvu ilikufanikisha malengo y etu, tunaweza kubadili matumaini kuwa uhalisia—yaani kutomwacha nyuma mtu yeyote.”

“Huu ni wakati muhimu wa matumaini duniani. Iwapo tutafanya kazi vizuri na kusalia kwenye mwelekeo pamoja tunaweza kuondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye lindi la umaskini na kupanua kwa kiasi kikubwa wigo wa hudum aza msingi ifikapo mwaka 2040 ambao ndio ukomo wa SDGs,” amesema mwenyekiti mwenza wa jopo hilo la SDGs na Rais wa Ghana Nana Addo Dankwa Akufo-Addo.   

Jopo hilo linajumuisha wajumbe 11 kutoka jopo la zamani na wajumbe sita wapya ili kusongesha SDGs.

Wachechemuzi 6 wapya ni:

  • Mfamle Muhammadu Sanusi II, Mtawala wa Kano nchini Nigeria.
  • Hindou Oumarou Ibrahim, mwanaharakati wa mazingira na watu wa asili kutoka Chad.
  • Dia Mirza, Muigizaji na mtengeneza filamu na pia balozi wa mwema wa shirika la mazingira duniani, UNEP na anatoka India.
  • Edward Ndopu, Muasisi wa mkakati wa kimataifa wa elimu jumuishi na anatoka Afrika Kusini.
  • Nadia Murad, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ambaye pia ni mwanzilishi na Rais wa mpango wa Nadia na balozi mwema wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya na uhalifu, yeye ni raia wa Iraq.
  • Marta Vieira da Silva, mcheza soka na balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen na ni raia wa Brazil.