Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa HLPF kuhusu SDG’s limeng'oa nanga leo: UN
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa HLPF kuhusu SDG’s limeng'oa nanga leo: UN
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu ,malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani chini ya mwamvuli wa baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC.
Jukwaa hilo ambalo litakunja jamvi 20 Julai mwaka huu limebeba maudhui “ "Kuharakisha kujikwamua kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19 na utekelezaji kamili wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu katika ngazi zote".
Mbali ya viongozi wa ngazi ya juu katikia jukwaa hilo kutakuwa na siku tatu za majadiliano katika ngazi ya mawaziri.
Kwa mujibu wa ECOSOC jukwaa hilo “litajumuisha mapitio ya mada ya malengo ya maendeleo endelevu namba 6 kuhusu maji safi na usafi wa mazingira, namba 7 kuhusu nishati nafuu na safi, namba 9 linalohusu viwanda, uvumbuzi na miundombinu, namba 11 linalohusu miji na jamii endelevu, na namba 17 linalohusu ubia kwa ajili ya malengo.”
Pia jukwaa hili ltashughulikia changamoto maalum zinazokabili nchi zilizo katika hali maalum.
Zaidi ya hapo litathimini vipimo vya kikanda na vya ndani ya nchi kuhusu kujikwamua kutoka kwaenye janga la COVID-19 na hali kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Na kisha litaunga mkono mapitio ya muda wa kati wa malengo ya SDGs na maandalizi ya mkutano wa mwa ka huu 2023 wa SDG mutaotarajiwa kufanyika Septemba.
Leo katika siku ya kwanza ya jukwaa hilo mada kuu zitakazopewa kipaumbele ni “kushinda majanga, kuleta mabadiliko kwa aajili ya SDGs, na kutomwacha mtu yeyote nyuma, Kufadhili hatua zetu za kukabiliana na majanga na kuwekeza katika SDGs.”
Nchi 39 zikiwemo Tanzania, Rwanda na Zambia zitafanya mapitio ya kitaifa ya hiari (VNRs) ya utekelezaji wao wa ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu katika katika jukwaa hilo la HLPF 2023.
Miongoni mwa wazungumzaji wa leo katika jukwaa hilo ni wasaidizi wa Katibu Mkuu Li Junhua, Qu Dongyu ambaye ni mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, Guy Ryder ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya sera, Mami Mizutori msaidizi wa Katibu Mkuu na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Msataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNDDR, na Filippo Grandi ambaye ni Kamisha mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.
Waliyoyasema
Katika hotuba yake kwa kongamano hilo, Rais wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC),
, amesema kuwa kongamano hilo "ni maalum kwani linatumika kama Mkutano wa Awali wa Mkutano wa SDG mnamo mwezi Septemba."
Amesema, "Mawazo yetu yatakuwa juu ya jinsi bora ya kuharakisha kupona kutoka kwa janga la COVID-19 na kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030. Hili ndilo lengo la mijadala yetu mwaka huu, na hatupaswi kulisahau.”
Stoeva ameendelea kusema, “Kama tunavyofanya kila mwaka, tutafanya mapitio ya kina ya Malengo kadhaa ya Maendeleo Endelevu. Mwaka huu, tutakuwa na vikao maalum kuhusu SDG namba 6 kuhusu maji safi na usafi wa mazingira, namba 7 kuhusu nishati nafuu na safi, namba 9 kuhusu viwanda, ubunifu na miundombinu, 11 kuhusu miji na jumuiya endelevu, na 17 kuhusu ushirikiano wa Malengo, pamoja na viunganishi vyake.”
Kwa upande wake Li Junhua, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, amesema, "Kiini cha mijadala yetu ni mapitio ya Hiari ya Kitaifa yaliyowasilishwa na nchi nyingi, kila moja ikionesha dhamira yao ya kuharakisha maendeleo ya SDG na kushiriki mafanikio yao na, wakati mwingine vikwazo.”
Amesema, "Tunafuraha kushuhudia ushiriki hai wa nchi 38, wanapowasilisha ripoti zao za mapitio ya kitaifa ya hiari (VNRs) na kukaribisha Mapitio ya Hiari ya kwanza ya Umoja wa Ulaya."
Wawakilishi 39 wanatarajiwa kuwasilisha Mapitio yao ya Kitaifa ya Hiari (VNRs) kuhusu utekelezaji wao wa Ajenda ya 2030 katika kongamano hili ni Bahrain, Barbados, Ubelgiji, Bosnia na Herzegovina, Brunei Darussalam, Burkina Faso, Kambodia, Canada, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Comoro, Chile, Kroatia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Muungano wa Ulaya, Fiji, Ufaransa, Guyana, Iceland, Ireland, Kuwait, Liechtenstein, Lithuania, Maldives, Mongolia, Poland, Ureno, Romania, Rwanda, Saudi Arabia, Singapore, Slovakia, St Kitts & Nevis, Tajikistan, Timor-Leste, Turkmenistan, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Uzbekistan, Vietnam na Zambia.
Kulingana na yeye, tangu 2015, nchi 188 zimefanya VNRs.
Li Junhua amesema, "Inatia moyo kuona kwamba nchi zimeboresha maandalizi yao, kushirikisha wadau kwa utaratibu zaidi na kutumia zana nyingi za uchambuzi."
Arrmanatha Christiawan Nasir, Makamu wa Rais wa Baraza la Uchumi na Kijamii na Mwakilishi wa Kudumu wa Indonesia kwenye Umoja wa Mataifa pia amehutubia kongamano hilo akisema, "Gonjwa hili na changamoto zake zinazoendelea linatukumbusha kila wakati juu ya uhusiano wake."
Amefafanua, "Zinaweza kushughulikiwa tu kupitia suluhisho zilizounganishwa, zana na mipango."
Kwa upande wake, Edward Ndopu, Mchechemuzi wa SDG na mwakilishi wa vijana, amesema, “Sisi ni wazawa wa kidijitali, wapiganaji wa tabianchi, wabunifu wa kijamii, sisi ndio waota ndoto na watendaji wa kesho iliyo bora zaidi. Na bado, mara nyingi sana, sauti zetu zinanyamazishwa. Michango yetu inapunguzwa uzito.
HLPF ni jukwaa kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu na ina jukumu muhimu katika ufuatiliaji na mapitio ya Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) katika ngazi ya kimataifa.