Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ya awali kwa watoto ni msingi wa mustakbali wao: UNICEF

wanafunzi wakionesha taa zinazotumia umeem wa jua zilizotolewa msaada wa Umoja wa Ulaya kuwawezesha kusoma nyakati za usiku
© UNHCR/Mohamed Aden Maalim
wanafunzi wakionesha taa zinazotumia umeem wa jua zilizotolewa msaada wa Umoja wa Ulaya kuwawezesha kusoma nyakati za usiku

Elimu ya awali kwa watoto ni msingi wa mustakbali wao: UNICEF

Utamaduni na Elimu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linashirikiana na wadau kuisaidia serikali ya Kenya katika kaunti ya Turkana kuhakikisha elimu ya awali inawafikia watoto wote hususan kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma. Flora Nducha anatupasha zaidi katika tarifa hii

Asubuhi mapema katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, ni wakati wa watoto kwenda shule tayari kuanza siku kwa masomo darasani “Mimi jina langu ni Nyota Plamedy Baraka nina miaka sita, napenda kusoma, napenda wageni , napenda vitabu na nawapenda marafiki zangu.”

Nyota ni miongoni mwa mamia ya watoto wakimbizi kutoka nchi mbalimbali walioko katika kambi hii na baba yake Baraka Munange mkimbizi mwenye watoto watano anasema elimu hii ni ya muhimu na ndio tegemeo pekee la mustakbali bora kwa watoto wao “Watoto wangu wanasoma shule ya msingi ya Morning Star , na shule ya chekechea ni nzuri sana kwa mwanzo wa mtoto kwa sababu inamfanya mtoto ajue kuongea, ajifunze kuandika na zaidi.”

Binti akiwa ameshikilia vitabu msaada wa Umoja wa Ulaya kwa watoto wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya
© UNHCR/Mohamed Aden Maalim
Binti akiwa ameshikilia vitabu msaada wa Umoja wa Ulaya kwa watoto wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya

Kambini hapa kuna shule nyingi ambazo kwa msaada wa ufadhili kutoka kwa kanisa la Jesus Christ of the Latter-day Saints Charities, UNICEF inaweza kuhakikisha elimu inatolewa ikiwepo katika shule ya msingi ya Kalemchuch “Jina langu ni Joyce Lotenga niña umri wa miaka 8, nasoma katika shule ya Kalemchuch.”

Joyce ni mmoja kati ya watoto tisa wa Francis Lomoi “Mimi ni babaye Joyce, Joyce yuko darasa la pili katika shule ya Kalemchuch kwa sababu tunakubali watoto wakimbizi kusoma pamoja na wengine, ili wote waweze kusoma kwenye shule pamoja ndio maana watoto wamekuwa wengi”

Watoto hawa wanafaidika na elimu chini ya program inayoendeshwa na serikali ya “Kujifunza Maisha yote” na mbali ya elimu pia wanashiriki shughuli mbalimbali za michezo ikiwemo kuimba.

Kwa mujibu wa serikali ya kaunti ya Turkana, ukame umekuwa changamoto kubwa kwa watoto hawa wanaotoka mataifa mbalimbali kupata elimu lakini jitihada zinafanyika.

Biti wa miaka 12 akiandika wakati wa kipindi cha sayansi daearasani kwenye kambi ya wakimbizi nchini Kenya
© UNHCR/Mohamed Aden Maalim
Biti wa miaka 12 akiandika wakati wa kipindi cha sayansi daearasani kwenye kambi ya wakimbizi nchini Kenya

Afisa wa elimu wa UNICEF Kenya Sarah Musengya paul anasela licha ya changamoto hizo “Hatua kubwa zimepigwa katika elimu ya awali kwenye kaunti ya Turkana, katika usaili wa watoto sasa ikiwa imefikia asilimia 166 ambayo ni juu ya kiwango cha wastan cha serikali, pili tumepiga hatua katika vifaa vya kusomea kama madawati na viti na vifaa vingine ambavyo vimewafanya wanafunzi kufurahia kuendelea kusoma. Lakini bado kuna changamoto katika kaunti ya Turkana ikiwemo mlo shuleni katika shule zinazotoa mlo kiwango bado ni kidogo hakikidhi mahitaji ya watoto hata wa chekechea.”

Kwa wazazi elimu hii inayotolewa ni baraka na matumaini kwa watoto wao “Mimi mzazi nikishakuja nyumbani nawakuta watoto wanazungumza walichofundishwa shuleni ni kiytu kimoja ambacho kinanifurahisha sana na kuonyesha kwamba watoto wanasoma vizuri.”

UNICEF limeahidi kuongeza juhudi zaidi hasa za kupata wafadhili ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa.