Chuo Kikuu cha wakimbizi kufunguliwa Kenya:UNHCR 

Kwa kuanzishwa Chuo hicho Kikuu cha Turkana, Esther Nyakong mwenye umri wa miaka 17 kutoka nchini Sudan Kusini, ataweza kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu.
UNHCR/Benjamin
Kwa kuanzishwa Chuo hicho Kikuu cha Turkana, Esther Nyakong mwenye umri wa miaka 17 kutoka nchini Sudan Kusini, ataweza kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu.

Chuo Kikuu cha wakimbizi kufunguliwa Kenya:UNHCR 

Wahamiaji na Wakimbizi

Umoja wa Mataifa unatambua kuwa wakimbizi nao licha ya kukimbilia ugenini kuokoa maisha yao, bado wana stadi mbalimbali na ujuzi ambao ukinolewa unaweza kuboresha siyo tu maisha yao bali pia maisha ya kule ambako wamesaka hifadhi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na uongozi wa jimbo la Turkana nchini Kenya wameshikamana ili kuanzisha Chuo Kikuu kipya kitakachotoa elimu ya juu kwa wakimbizi kwenye kambi ya Kakuma Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkakati wa ujenzi wa chuo hicho kitakachoitwa  Chuo Kikuu cha Turkana West umezinduliwa Jumatatu kambini Kakuma mbele ya umati wa wakimbizi na raia wa Kenya wanaoishi karibu na eneo hilo.

Wengine waliokuwepo ni pamoja na mwakilishi wa UNHCR Kenya Raouf Mazou,  Naibu Gavana wa Turkana na maafisa wengine wa serikali.

Kwa mujibu wa UNHCR chuo hicho  kitatoa mafunzo mbalimbali yakiwemo yangazi ya diploma na shahada au degree na mafunzo hayo yataandaliwa na kuendeshwa na chuo kikuu cha Masinde Muliro ambacho ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimika sana nchini Kenya.

Bwana Mazou amesema lengo na matumaini ya UNHCR kwamba chuo icho kitatatoa fursa ya kusoma na elimu ya juu kwa wakimbizi nlakini pia raia wa Kenya kwa gharama nafuu wanayoweza kuimudu.

Ameongaza kuwa hali hiyo itadhihirishatalanta, vipaji na mchango wa wakimbizi kwa maisha yao, jamii zinazowahifadhi na hata kusaidia kule walikotoka.

Naye naibu gavamna wa Turkana , Peter Lotethiro amesema raia wa Turkana wamekaribisha kwa mikono miwili mpango wa ujenzi wa chuo hicho ambacho malengo yake yanaungwa mkono kikamilifu na serikali ya Kenya.