Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Türk: Kupambana na mabadiliko ya tabianchi kutalinda haki ya chakula

Ukame umeharibu ardhi kusini mwa Ethiopia na ndio chanzo kikuu cha vifo vya mifugo.
© WFP/Michael Tewelde
Ukame umeharibu ardhi kusini mwa Ethiopia na ndio chanzo kikuu cha vifo vya mifugo.

Türk: Kupambana na mabadiliko ya tabianchi kutalinda haki ya chakula

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk ametoa onyo kali kuhusu hatari ya mabadiliko ya tabianchi kwa haki ya watu kupata chakula akisema “Mazingira yetu yanaungua, yanayeyuka, mafuriko na vyanzo vya maji vinakauka na kufa kabisa."

Akizungumza katika kikao cha 53 cha Baraza la Haki za Kibinadamu huko Geneva, Uswisi Türk amesema, “Mabadiliko ya kawaida ya misimu yaliyokuwa yakitabirika sasa hayatabiriki, vimbunga vya idadi isiyo na kifani huchochea mawimbi ya dhoruba hatari, mawimbi ya joto hutiririka baharini, na kutishia viumbe vya baharini, uvuvi na matumbawe, na maziw, ambayo yamekuza kizazi kwa kizazi vya wakulima, yanageuka kuwa bakuli za vumbi.”

Amesema pamoja na juhudi zinazochukuliwa lakini ukweli ni kuwa bado wanadamu hawafanyi kazi kwa uharaka na azma inayohitajika. Viongozi nao amesema wanatekeleza utaratibu wa kuamua kuchukua hatua na kuahidi kuchukua hatua na kisha kukwama katika muda mfupi.

"Katika mkondo wetu wa sasa, wastani wa ongezeko la joto kufikia mwisho wa karne hii itakuwa nyuzi joto 3 ° Selsiasi, na mifumo yetu ya ikolojia - inayohusisha hewa yetu, chakula chetu, maji yetu, na maisha ya binadamu yenyewe - haitambuliki," Türk alisema.

Ametolea mfano mwezi Agosti 2022, halijoto huko Basrah, kusini mwa Iraq, ilipanda hadi nyuzi joto 52.6° Selsiasi na kusema tasafiri Kwenda nchini Iraq baadaye mwaka huu,ili kujionea hatari za siku zijazo.

Nini kifanyike?

Ikiwa tutakomesha ruzuku zisizo na maana kwenye sekya ya mafuta na kuanza kumaliza nishati ya mafuta. Iwapo tutatekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi mwaka 2022 COP28 kuwa mbadiliko madhubuti tunayohitaji sana basi dunia inaweza kukabiliana na changamoto za ukosefu wa chakula amesema kamishna Turk.

Kamishna Mkuu ameeeleza kwa kina hatua nyingine zinazohitajika ikiwa ni pamoja na : 

  1. Mahakama duniani kote ambazo zinahusika na kesi za madai ya tabianchi lazima ziwajibishe wafanyabiashara na Serikali.
  2. Kujiepusha na wasiependa maendeleo ya kijani na kutilia juu ya ushahidi na ukweli, kwa uchoyo wao wenyewe. 
  3. Kushinda nguvu za ubaguzi, na kuungana karibu na kwa umuhimu katika harakati za haki za binadamu.

Türk pia ilionesha hitaji la kubadilisha taasisi za maendeleo ya kimataifa na ufadhili kuwa injini za hatua za hali ya hewa, ili nchi na watu walioathiriwa zaidi wapate ufadhili kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo alitoa angalizo kuwa hatua za kuzingatia utawala bora lazima zichukuliwe, ili ufadhili unapopatikana, ulete msaada, na tiba kwa watu walioathirika zaidi. Kisha mabadiliko ya haki kwa uchumi wa kijani - kitaifa, na kimataifa - yanaweza kutokea.

“Tunaweza kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu. Tunaweza kutambua haki yetu ya chakula kwa wote. “

“Tunaweza kutetea haki yetu ya mazingira safi, yenye afya na endelevu. Tunaweza. Kwa sababu bado kuna wakati wa kutenda. Lakini wakati huo ni sasa. Hatupaswi kuacha hili kwa watoto wetu kurekebisha - bila kujali jinsi uharakati wao unavyochochea. Watu ambao wanapaswa kuchukua hatua - ambao wana jukumu la kuchukua hatua - ni viongozi wetu, leo," alisema.

"Ninaomba kila mjumbe wa Baraza hili atoe ujumbe huu wazi kutoka katika mkutano huu hapa Palais des Nations na katika kila nyanja ya kazi yao. Kushughulikia mabadiliko ya tabinachi ni suala la haki za binadamu. Dunia inadai hatua sasa,” alisema Turk akihitimisha hotuba yake.

Haki ya chakula na hali ya hewa

Baraza la haki za binadamu hii leo lililikuwa likijadili haki ya chakula na Kamishna huyo wa UN amesema haki hiyo inatishiwa na mabadiliko ya tabianchi, na maafa ya ghafla na ya polepole yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, huangamiza mazao, mifugo, uvuvi na mifumo yote ya ikolojia.

Hali hiyo ikiachwa iendelee jumuiya nyingi zitalazimika kujijenga upya ili ziweza kujikimu Kurudiwa kwao kunafanya kutowezekana kwa jumuiya kujijenga upya na kujikimu alisema Türk.

Ulimwenguni kote, kumekuwa na ongezeko la asilimia 134 la majanga yanayosababishwa na hali ya hewa, yanayohusiana na mafuriko kati ya mwaka 2000-2023.

Zaidi ya watu milioni 828 walikabiliwa na njaa mwaka wa 2021. Na mabadiliko ya hali ya hewa yanakadiriwa kuweka hadi watu milioni 80 zaidi katika hatari ya njaa katikati mwa karne hii - na kuunda kiwango cha kutisha cha kukata tamaa na mahitaji.

Tayari, kulingana na Jopo la Serikali Mbalimbali la Mabadiliko ya Tabianchi, hali mbaya ya hewa inayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa imeharibu tija ya sekta zote za kilimo na uvuvi, na matokeo mabaya kwa usalama wa chakula na maisha ya watu. 

Hivi sasa, athari hii ni mbaya zaidi kwa wakulima wadogo, na kwa watu wa Afrika katika ukanda wa Sahara, Kote barani Asia, katika Nchi za Visiwa vidogo, na Amerika ya Kati na Kusini.