Ujumbe wa jeshi la wananchi la Tanzania watembelea vikosi vya FIB nchini DRC
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Brigedia Jenerali Geoge Mwita Itang’are akiwa ameambatana na ujumbe wake kutoka makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania (JWTZ) kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Tanzania Jenerali John Jacob Mkunda umefanya ziara ya kutembelea makao makuu ya majeshi ya Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO kwenye eneo la Goma na kukutana na kamanda wa vikosi hivyo Luteni Jenerali Otavio Rodrigues De Miranda Filho.