JWTZ

30 Oktoba 2019

Hii leo jaridani, Arnold Kayanda anaanza na ripoti za uzinduzi wa kamati ya kikatiba kwa taifa la Syria huko Geneva, Uswisi! Imeelezwa kuwa ni tukio la historia.

Sauti -
9'56"

Sasa mkirudi nyumbani, wale watakaokuja huku muwaeleze waendelee kutusaidia- Mnufaika wa mafunzo DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mafunzo ya ufundi cherehani yaliyotolewa na walinda amani wanawake kutoka Tanzania kwa wanawake wakazi wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini yameanza kuleta matumaini na kudhihirisha jukumu la ulinzi wa amani na uwezeshaji wa jamii nchini humo.

Ufundi cherehani na upanzi wa mboga ni mkombozi kiuchumi kwa wanawake DR

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mafunzo ya ufundi cherehani yaliyotolewa na walinda amani wanawake kutoka Tanzania kwa wanawake wakazi wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini yameanza kuleta matumaini na kudhihirisha jukumu la ulinzi wa amani na uwezeshaji wa jamii nchini humo.

Sauti -
2'15"

Tunachangia sana walinzi wa amani na sasa tutaongeza idadi ya wanawake- Luteni Jenerali Yacoub Mohamed JWTZ

Mkutano wa nchi zinazochangia vikosi vya ulinzi wa amani, TCCF, umekunja jamvi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjini New York Marekani

Jeshi la wananchi Tanzania, JWTZ lanuia kutekeleza lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa vitendo.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora, unapigia chepuo elimu ambayo si tu jumuishi bali pia inampatia mnufaika stadi za kumkomboa kimaisha, iwe kwa kupata ajira akiwa ofisini au akiwa kwenye medani za nje.

Sauti -
4'53"

Jeshi la wananchi Tanzania, JWTZ lanuia kutekeleza kwa vitendo lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora, unapigia chepuo elimu ambayo si tu jumuishi bali pia inampatia mnufaika stadi za kumkomboa kimaisha, iwe kwa kupata ajira akiwa ofisini au akiwa kwenye medani za nje. Nchini Tanzania, moja ya mataifa yaliyoridhia malengo hayo, jeshi la wananchi, JWTZ limeitikia wito huo kupitia shule ambazo inazimiliki. Luteni Kanali Semunyu wa JWTZ alishiriki kikao kilichosheheni maofisa wa ngazi mbalimbali za kijeshi pamoja na wale wanaoongoza taasisi za elimu zilizoko chini ya JWTZ.

FIB inasema UN inauwezo wa kutuliza mambo DRC

Kikosi maalumu kilichoanzishwa na Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa ajili ya kufurusha makundi ya waasi na kujibu mashambulizi (FIB) kinakabiliwa na changamoto nyingi, japo imani ipo kwamba Umoja wa Mataifa utazitatua.

Sauti -
1'57"

Nina Imani UN itatatua changamoto zinazoikabili :FIB