Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yataka hatua madhubuti zichukuliwe kufuatia ajali ya meli nchini Ugiriki

Ajali kubwa zaidi ya meli kuwahi kutokea katika historia ya Ugiriki imesababisha vifo vya mamia ya watu.
IOM/Amanda Nero
Ajali kubwa zaidi ya meli kuwahi kutokea katika historia ya Ugiriki imesababisha vifo vya mamia ya watu.

UN yataka hatua madhubuti zichukuliwe kufuatia ajali ya meli nchini Ugiriki

Wahamiaji na Wakimbizi

Baada ya ajali mbaya ya meli katika pwani ya Ugiriki iliyotolewa Jumatano 14, Juni 2023, ambayo imesababisha vifo vya takriban watu 78, na mamia ya watu bado hawajulikani waliko mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yametoa wito wa kuchukua hatua za haraka na Madhubuti kuzuia janga kama hilo kutokea tena.

Kwa mujibu wa UNHCR, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, lengo ni kuepusha vifo zaidi baharini kufuatia janga la hivi karibuni katika bahari ya Mediterania.

Federico Soda, mkurugenzi wa idara ya dharura ya IOM, katika taarifa yake amesema "Janga hili ni baya zaidi kuwahi kutokea katika miaka kadhaa. Ni wazi kuwa mtazamo wa sasa kwa bahari ya Mediterania hauwezi kufikiwa. Mwaka baada ya mwaka, inasalia kuwa njia hatari zaidi ya uhamiaji duniani, yenye kiwango cha juu zaidi cha vifo.” 

Idadi ya watu waliokuwa kwenye boti hiyo iliyopinduka tarehe 14 Juni katika pwani ya Ugiriki haijulikani. 

Lakini kulingana na Umoja wa Mataifa, tarifa za mashuhuda itakuwa "kati ya wahamiaji 400 na 750".

"Ni wazi kuwa njia ya sasa ya Bahari ya Mediterania haiwezi kufikiwa. Mwaka baada ya mwaka, inasalia kuwa njia hatari zaidi ya uhamiaji duniani, yenye kiwango cha juu zaidi cha vifo.”

Mamia ya watu bado hawajulikani waliko 

Kufikia sasa, watu 104 wameokolewa na miili 78 imeopolewa, huku mamia ya watu bado hawajulikani walipo na wanahofiwa kufa maji.

Kwa mujibu wa tarifa ya IOM mashua hiyo ilikuwa na matatizo tangu asubuhi ya Juni 13. 

Operesheni kamili ya utafutaji na uokoaji ilitangazwa na walinzi wa pwani ya Ugiriki asubuhi ya Juni 14, baada ya mashua hiyo kupinduka.

Wakati UNHCR na IOM zikikaribisha uchunguzi ambao umeamriwa nchini Ugiriki kuhusu hali iliyosababisha kupinduka kwa meli hiyo na kupoteza maisha ya watu wengi, mashirika hayo mawili yamekumbusha kwamba "jukumu la kuwaokoa watu bila kuchelewa katika dhiki bahari ni ni kanuni ya msingi ya sheria za kimataifa za baharini”.

Yameongeza kuwa njia moja ya kukumbuka ni kwamba manahodha wa meli na mataifa wana wajibu wa kutoa msaada kwa watu walio katika dhiki baharini, bila kujali utaifa wao, hali yao au hali ambayo wanajikuta, ikiwa ni pamoja na kwenye meli ambazo hazistahili kusafirishwa, bila kujali nia ya walio kwenye meli.

Utafutaji na uokoaji baharini ni sharti la kisheria na la kibinadamu

Gillian Triggs, kamishna mkuu msaidizi wa ulinzi wa UNHCR kwa upande wake amesema "Nchi lazima ziungane na kuziba mapengo katika utafutaji na uokoaji makini, kushuka kwa haraka kwa manusura na njia salama za kawaida. Juhudi hizi za pamoja lazima zizingatie haki za binadamu za wahamiaji na kuokoa maisha ya binadamu.” 

Ameongeza akibainisha kuwa hatua zozote za utafutaji na uokoaji lazima zifanyike kwa kuzingatia wajibu wa kuzuia kupoteza maisha ya watu baharini.

UNHCR na IOM wanakumbusha kwamba utafutaji na uokoaji baharini ni jambo la lazima kisheria na la kibinadamu. 

"Muungano wa Ulaya EU, lazima uweke usalama na mshikamano katika kitovu cha hatua zake kwenye baharí ya  Mediterania," 

Kwa kuzingatia ongezeko la harakati za wakimbizi na wahamiaji katika bahari ya Mediterania, UNHCR inaamini kwamba juhudi za pamoja, ikiwa ni pamoja na uratibu zaidi kati ya mataifa yote ya Mediterania na kugawana majukumu, ni muhimu kuokoa maisha. 

"Hii ni pamoja na kuanzishwa kwa utaratibu wa kikanda wa kushusha manusura na ugawaji upya kwa watu wanaowasili kwa njia ya bahari, ambayo tunaendelea kutetea," Bibi Triggs aliongeza.

Mkimbizi akilala kifudifudi kwenye ardhi yenye mawe baada ya kufika ufukweni, karibu na kijiji cha Skala Eressos, kwenye kisiwa cha Lesbos, katika eneo la Kaskazini mwa Aegean nchini Ugiriki.
Picha: UNICEF/Ashley Gilbertson VII
Mkimbizi akilala kifudifudi kwenye ardhi yenye mawe baada ya kufika ufukweni, karibu na kijiji cha Skala Eressos, kwenye kisiwa cha Lesbos, katika eneo la Kaskazini mwa Aegean nchini Ugiriki.

Janga la kutisha-OHCHR

Kwa upande wake, Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imedokeza kwamba hasara ya kutisha ya maisha ya binadamu katika bahari ya Mediterania ni janga la kutisha. 

"Kilichotokea Jumatano kinasisitiza haja ya kuwachunguza wasafirishaji wa binadamu na wasafirishaji haramu na kuhakikisha wanafikishwa mahakamani," Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi.

Volker Türk, ameelezea mshikamano wake na walionusurika na familia za walioathirika katika ajali hiyo.

Kamishna mkuu pia amesisitiza wito wake kwa Mataifa kufungua njia zaidi za uhamiaji za mara kwa mara, kuimarisha ugawanaji wa uwajibikaji, kufanya mipango ya kuteremka salama kwa wahamiaji hao kutoka melini na haraka kwa watu wote waliookolewa baharini. Pia amesema inahusu kuweka hatua za ufuatiliaji na udhibiti huru wa sera na desturi zinazohusiana na uhamiaji.

Tangu mwanzo wa mwaka huu hadi kufikia 11 Juni 2023, angalau wahamiaji 72,778 wamewasili Ulaya miongoni mwao wahamiaji  54,205 nchini Italia pekee kupitia njia za wahamaji Mashariki, Kati, na Magharibi mwa Mediterania au kupitia Afrika Kaskazini-Magharibi kulingana na takwimu zilizochapishwa na IOM. 

Wakati huo huo, takriban wahamiaji 1,037 wamekufa au kupotea wakijaribu kuvuka kupitia bahari hiyo ya Mediterrania kuingia Ulaya.