Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki unafikisha ujumbe wa haki za binadamu: Robdarius 'Roben X' Brown

Mwanamuziki na mwanaharakati RobenX (katikati), akiwa na watazamaji kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Haki za Kibinadamu kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva. 12 Desemba 2018.
UN Photo/Violaine Martin
Mwanamuziki na mwanaharakati RobenX (katikati), akiwa na watazamaji kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Haki za Kibinadamu kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva. 12 Desemba 2018.

Muziki unafikisha ujumbe wa haki za binadamu: Robdarius 'Roben X' Brown

Haki za binadamu

Kuanzia umri mdogo, Robdarius Brown, jina la kisanii Roben X, alivumilia uonevu kwa sababu ya Ualbino wake. Muziki ni sehemu muhimu ya maisha ya Roben X na imekuwa njia yake ya kupunguza maumivu yake na kupata kujiamini. 

Katika mji aliozaliwa wa Memphis, Tennessee, Marekani, anaelimisha watu kuhusu ualbino na mara kwa mara anatembelea shule ili kufanya mazunumzo ya kuwatia moyo wanafunzi wachanga dhidi ya unyanyasaji. Hadithi ya maisha yake ni ya kujiamini, kujithamini, na kukubali utambulisho wake wa kipekee. 

Rapa na mwanaharakati RobenX, katika mahojiano na UN News kabla ya onyesho la kuadhimisha Siku ya Haki za Binadamu katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva. 12 Desemba 2018.
UN Photo/Elma Okic
Rapa na mwanaharakati RobenX, katika mahojiano na UN News kabla ya onyesho la kuadhimisha Siku ya Haki za Binadamu katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva. 12 Desemba 2018.

Akiwa ni  mmoja wa Mabingwa wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, kijana huyu kupitia mazungumzo yake na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Roben X anaeleza kuhusu mapito ya maisha yake.

“Nimeonewa nusu ya maisha yangu yote,” ndivyo anavyoanza kueleza Robdarius Brown au Roben X kuhusu maisha yake ambayo kwa kiasi kikubwa ni sawa na hali wanayokabiliana nayo watu wengine wenye ualbino duniani kote.  

Anasema…alianza kwa kupewa majina mabaya, kusukumwa na pia manyanyaso mengine kama kupigwa mateke. Kwa ufupi alinyanyasika sana katika kukua kwake kisa tu yeye ana ualbino.  Anasema alifikia wakati hata kutaka kujiua na alijisikia mpweke na kwa kweli kwa sasa jambo ambalo asingependa kumfanyia mtu mwingine ni kumfanya ajisikie mpweke.  

Roben X anaendelea kueleza akisema, “Kama unavyoona, mimi ni albino. Sina rangi zote kwenye nywele, ngozi, macho, na nina aina maalum ya ualbino inayoitwa ocular albinism au ualbino wa macho. Kwa hivyo, sina rangi ya asili yoyote. Nililelewa katika mtaa wenye watu weusi wengi na shule yenye watu weusi. Na watoto, unajua, hawajui jinsi ya kukabiliana na kitu ambacho ni tofauti sana. Na mambo yalianzia hapo.” 

Ualbino ni hali ya kimaumbile inayorithiwa kutoka kwa wazazi wote wawili ambayo hutokea duniani kote, bila kujali kabila au jinsia. 

Ukosefu wa kawaida wa rangi ya melanini kwenye nywele, ngozi na macho ya watu wenye ualbino husababisha hatari ya jua kupeya moja kwa moja kwenye ngozi zao na hali hiyo inaweza kusababisha saratani ya ngozi na ulemavu mkubwa wa macho. 

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema takribani mtu 1 kati ya watu 5,000 katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na mtu 1 kati ya watu 20,000 barani Ulaya na Amerika Kaskazini wana ualbino. 

 Rapa na mwanaharakati RobenX (kulia), wakati wa mahojiano na Daniel Johnson wa UN News (kushoto), kabla ya onyesho la kuadhimisha Siku ya Haki za Kibinadamu kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva. 12 Desemba 2018.
UN Photo/Elma Okic
Rapa na mwanaharakati RobenX (kulia), wakati wa mahojiano na Daniel Johnson wa UN News (kushoto), kabla ya onyesho la kuadhimisha Siku ya Haki za Kibinadamu kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva. 12 Desemba 2018.

Katika baadhi ya nchi watu wenye ualbino wanakabiliwa na ubaguzi, umaskini, unyanyapaa, ukatili na hata mauaji. Ndio maana kijana huyu Roben X anatumia kipawa chake cha muziki kuepelea ujumbe kwa jamii, “Ndiyo, ni jukwaa ninalotumia kuwasiliana vyema na rika langu na vijana. Ninazungumza, lakini wakati mwingine kuzungumza tu hakufanyi kazi. Muziki husaidia kupenya.” 

Anaendelea kueleza kwamba,“Halafu unapozaliwa, ukiwa mtoto hujui chuki, hujui maumivu, hujui ubaguzi. Hayo unafundishwa. Mambo hayo tunafundishwa sisi watoto. Tukiondoa vitu kwa vijana wetu vinavyofundisha aina hiyo ya chuki na kuacha kubagua, tukapendana tu. Na tunaweza kufundisha upendo kwa vijana wetu na kufundisha upendo kwa watu wetu na kuendelea kufundisha hilo katika jumii zetu. Ndpo kutakuwa na mabadiliko. Hatimaye. Hilo lingetufanya tushiriki zaidi kama watu kwenye mazingira na kupata viongozi wengi zaidi wa kuendelea kusukuma upendo huo na amani hiyo na kujali wengine.” 

Soundcloud

Anahitimisha kwa kusema, “Simama kwa ajili ya Haki za Binadamu.”