Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makazi ni moja ya changamoto kubwa kwa jamii ya watu wa asili wa Inuit wa Eskimo: Nakimayak

Herbert Angiki Nakimayak,Makamu wa rais wa baraza la jamii ya Inuit nchini humo anayehudhuria jukwaa la 22 la watu wa asili la Umoja wa Mataifa hapa Marekani alipozungumza na Idhaa hii ya Kiswahili.
UN News
Herbert Angiki Nakimayak,Makamu wa rais wa baraza la jamii ya Inuit nchini humo anayehudhuria jukwaa la 22 la watu wa asili la Umoja wa Mataifa hapa Marekani alipozungumza na Idhaa hii ya Kiswahili.

Makazi ni moja ya changamoto kubwa kwa jamii ya watu wa asili wa Inuit wa Eskimo: Nakimayak

Haki za binadamu

Jamii ya Inuit ya watu wa asili wa Eskimo ni miongoni mwa jamii za walio wachache sana kutoka jimbo la Inuvik nchini Canada. Jamii hiyo ambayo ina jumla ya watu 180,000 kwa asili ni ya wawindaji, wavuvi na wafugaji wa kuhamahama, lakini sasa kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi wamelazimika kubadili mfumo wa maisha na kuishi mahali pamoja katika vijiji.

Hata hivyo mabadiliko hayo yamewaletea changamoto kubwa kama anavyosema Herbert Angiki Nakimayak makamu wa rais wa baraza la jamii ya Inuit nchini humo anayehudhuria jukwaa la 22 la watu wa asili la Umoja wa Mataifa hapa Marekani alipozungumza na Idhaa hii ya Kiswahili,

“Nyumba siku zote imekuw ni changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika maeneo ya vijijini na tunafanyakazi kwa karibu na uongozi ili kuhakikisha kwamba tuna nyumba zinazojitosheleza ili familia zetu ziewe kukuwa pamoja na kuwa zenye afya. Pia sidhani kama nchi au serikali zimejikwamua vyema kutoka kwenye janga la COVID-19, hivyo kuna huduma ambazo hazipatikani kwa watu wa jamii ya asili ya Inuit. Na baharini tuna msongamano wa meli ndogo na kubwa , pia linapokuja suala la umwagaji wa mafuta  hatuna uwezo wa kukabiliana nalo hali itakayoathiri uhamaji wa viumbe kama nyangumi na samaki , Ndege na bata maji ambao wanahama ambao tunawtegemea.”

Nakimayak ameongeza kuwa changamoto hizo anaamini suluhu itapatikana endapo jamii husika za asili zitajumuishwa na huo ndio ujumbe aliouleta kwenye jukwaa hili la watu wa asili, 

“Serikali , nchi na mataifa wanaandaa será na sheria kwa asili ya watu wa asili, lakini sasa wakati umefika kwa nchi hizo kufanyakazi na watu wa asili ili kuunda sheria na taratibu kwa ajili ya watu wa jamii zetu hasa wa vijijini ambao hawawakilishwi vya kutosha.”

Na kwa jumuiya ya kimataifa ana wito, 

“Tungependa nchi na wanasayansi kuelewa kwamba sisi ni sehemu ya mfumo wa maisha na chochocte kitakachotokea katika mfumo wa maisha baharini au nchi kavu kitatuathiri pia, kitaathiri afya zetu na uwezo wetu wa kuendelea na mfumo wetu wa maisha wa kitamaduni na tunataka kulinda hilo kwa kadri tuwezavyo. Tunataka kuhakikisha kwamba tunalinda utamaduni wetu kwa ajili ya leo, kesho na wakati ambao watunga será na sheria watakapokuja kuweka sheria, será na kanuni ili wanafanye hivyo pamoja nasi na kwa ajili yetu hivyo ujumuishwaji ni ufunguo.”