Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia inaleta tija kwa wanawake wakulima nchini Kenya: Husna- FAO

Husna Mbaraka, afisa msimamizi wa masuala ya ardhi, maliasili na jinsia wa FAO nchini Kenya akizungumza na Flora Nducha jijini New York Marekani.
UN News
Husna Mbaraka, afisa msimamizi wa masuala ya ardhi, maliasili na jinsia wa FAO nchini Kenya akizungumza na Flora Nducha jijini New York Marekani.

Teknolojia inaleta tija kwa wanawake wakulima nchini Kenya: Husna- FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO nchini Kenya linafanya kila juhudi kuhakikisha linatimiza wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka ubunifu na teknolojia vitumike kama nyenzo ya kumuinua mwanamke  kiuchumi na kijamii lakini pia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs na kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma kwenye zama hizo za kidijitali.

Soundcloud

Shirika hilo limeanzisha miradi mbalimbalimbali jumuishi kwa lengo la kuwasaidia wanawake hasa wakulima nchini humo , Husna Mbaraka afisa msimamizi wa masuala ya ardhi, maliasili na jinsia wa FAO nchini Kenya akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amesema “ Kuna maeneo mawili ambayo FAO inaisaidia nchi ya Kenya , moja ni kuweka mifumo kuhakikisha kuna taarifa kuhusuiana na suala la kilimo , lengo la mifumo hiyo ni kuhakikisha wakulima wameweza kusajiliwa , lkama tunavyojua Kenya nan chi nyingi duniani zinafanya ukulima wa hali duni na hasa mashinani hivyo tunahakikisha kuwa wamesajiliwa na kuweza kupata huduma tofautitofauti kupitia mfumo huo.”

Pili amesema ni “Mfumo huu hauangalii suala la usajili peke yake bali pia ni kuhakikisha tunajua ardhi gani ipo, ardhi gani imeweza kusajiliwa na ardhi gani inaweza kutumika na kwa namna gani kwa upande wa kilimo, hivyo tunashirikiana na serikali ya Kenya na mifumo hiyo haibagui lakini kinachopendekezwa zaidi ni kuhakikisha mwanamke anajulikana anafanya nini , anafanya ukulima , pili ilia pate huduma sawasawa na kingine ni kuhakikisha mwanamke anapata fursa ya juu katika suala la utumiaji na umiliki wa ardhi.”

Husna Mbaraka afisa msimamizi wa masuala ya ardhi, maliasili na jinsia wa FAO nchini Kenya akizungumza na Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.
UN News
Husna Mbaraka afisa msimamizi wa masuala ya ardhi, maliasili na jinsia wa FAO nchini Kenya akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Mwanamke hajaachwa nyuma kidijitali

Bi. Mbaraka amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia “nafikiri dunia nzima sasa watu wanatumia simu za rununu hivyo katika mfumo huo uliowekwa tunahakikisha mwanamke ameweza kusajiliwa nan amba yake ya simu kisha kuna huduma , ujumbe wa simu ambao wanaweza kuupata ambao unawauliza pia mbali ya kusajiliwa wangependa kupatiwa huduma gani mfano kama wangehitaji mbolea ule ujumbe unaweza kutumwa nao wakajibiwa , na pia endapo kuna msaada wowote umetokea katika suala la elimu wanapata ujumbe . Lakini muhimu pia Kenya inatoa kipaumbele katika kilimo biashara mfano utumiaji wa M-Pesa hivyo huduma hiyo ikiwa mahali ambapo mwanamke yuko inakuwa rahisi na anaweza kupata hizo huduma hata akiwa shambani kwake.”

Akaenda mbali zaidi na kusema kwamba huduma hizo pia zinawapa fursa wakulima kutambua kwamba ardhi hiyo ni nzuri kwa kilimo cha aina gani na kwa wakati gani.

Teknolojia inachangamoto zake kwa wakulima

Afisa huyo wa FAO amesema pamoja na jitihada zote zinazofanyika lakini bado sio kila mtu anayefaidika na maendeleo hayo ya teknolojia “Changamoto bado zipo kwa sababu kila uchao teknolojia inabadilika mfano mama anaweza kuwa na simu lakini simu inayohitajika kutambua ile mifumo ni simu janja au smartphone, hivyo wanapata kidogo changamoto ya kupata huduma zaidi sababu wengi wao simu zao ni zile za kawaida. Pia ukiangalia idadi ya waliosoma bado kuna changamoto kidogo upande wa wanawake kwani Kenya na Afrika kwa ujumla idadi ya waliosoma zaidi ni ya wanaume na pia lugha katika simu hizo janja wasichana wanaelewa zaidi kuliko wanawake wenye umri mkubwa hivyo lazima kuwe na taaluma kidogo, mafunzo na uhamasishaji wa utumiaji wa hiyo teknolojia.”

Nini kifanyike kutomwacha mwanamke mkulima nyuma

Katika kuhakikisha kila mwanamke anajumuishwa hasa mkulima wa kijijini na kutoachwa nyuma kidijitali Bi. Mubaraka anasema kuna masuala ya kuzingatia “Kwanza kabisa ni kuhakikisha sera na sheria za kitaifa zinatambua hilo na kuliweka kuwa kama ni sheria na ili zifuatwe kwa Kenya tumona kuna kipengelekimewekwa katika katiba cha kuhakikisha kuna idadi kamili ya watu wanaojumuishwa katika kamati ay taasisi za kiserikali na kijamii, na inakuwa changamoto sana kama haiku kisheria, pili ni kuhamasisha jinsia zote hasa katika masuala ya kilimo hasa tukitambua kuwa wazalishaji wakubwa wa kilimo hasa Afrika ni wanawake hivyo kulitambua hilo na kuhakikisha ile huduma na misaada inayotakikana hasa kwa mwanamke aweze kupata . Pia uhamasishaji lazima uendelee katika kila tunalofanya kuhakikisha watu wanatambua kuwa mke na mume ni sawa kwa njia zote, na kutambua kila mtu sehemu yake katika jamii na hilo ni muhimu zaidi.”