Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN ataja vipaumbele vyake kwa mwaka 2023

Katibu Mkuu António Guterres (katikati) akitembelea vitongoji vya makazi ya Irpin, katika Kyiv Oblast ya Ukraine.
UN Photo/Eskinder Debebe
Katibu Mkuu António Guterres (katikati) akitembelea vitongoji vya makazi ya Irpin, katika Kyiv Oblast ya Ukraine.

Katibu Mkuu wa UN ataja vipaumbele vyake kwa mwaka 2023

Masuala ya UM

Wakati unazidi kusonga huku dunia ikikaribia kuyeyuka na nchi zinapaswa kubadilika bila kuchelewa ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo wakati akiwasilisha vipaumbele vyake vya mwaka 2023.

Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Guterres ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka hivi sasa ili kuweza kufikia amani, haki za kiuchumi na maendeleo, hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuheshimu tofauti, na kuwa na jamii jumuishi -sasa na kwa vizazi vijavyo.

Kabla ya kuainisha ramani yake ya mwaka 2023, Katibu Mkuu alituma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa maafa ya matetemeko la ardhi huko Türkiye na Syria, akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa unahamasisha na unashiriki juhudi za uokoaji.

Mbinu inayozingatia haki

Kisha akaanza kutaja vipamele vyake ambapo alisisitiza haja ya mageuzi mwaka huu, msingi wake ukitoka katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu.

"Tunapotazama vipaumbele vya mwaka huu, mtazamo unaozingatia haki ni msingi wa kufikia kipaumbele chetu kikuu: ulimwengu ulio salama, wa amani zaidi na endelevu," alisema Katibu Mkuu Guterres na kuongeza kuwa azimio hilo  “Linaelekeza njia ya kutoka kwenye mwisho mbaya wa leo. Ni lazima tuchukue hatua - na kuchukua hatua madhubuti kabla hatujachelewa."

Saa ya Siku ya Mwisho inakaribia

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa kwa kurejelea habari kwamba Saa ya Siku ya Mwisho - ilitengenezwa miaka 75 iliyopita na wanasayansi wa atomiki kupima ukaribu wa wanadamu hadi usiku wa manane, au kujiangamiza  ilikuwa sekunde 90 tu kutoka saa hiyo.

Uvamizi uliofanywa na Urusi nchini Ukraine, hali ya dharura kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa vitisho vya nyuklia, na kudhoofisha kanuni na taasisi za kimataifa kumesukuma ulimwengu karibu na maangamizi.

"Hii ndiyo saa iliyo karibu zaidi kuwahi kusimama kwa saa ya giza zaidi ya wanadamu,  karibu zaidi kuliko hata wakati wa kilele cha Vita Baridi. Kwa kweli, Saa ya Siku ya Mwisho ni saa ya kengele duniani kote. Tunahitaji kuamka - na kuanza kazi," alisema.

Tufikirie kesho

Akisisitiza kwamba "tunahitaji kufanya  marekebisho ", mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema hatua zipo na zinawezekana, hata hivyo wanasiasa na wafanya maamuzi wanakosa dira ya kimkakati ya kuona zaidi ya muda mfupi.

"Kinachopendelea kwa sasa na wengi “ni maamuzi yanayolenga tu uchaguzi unaofuata, mwendo kasi, au mzunguko wa biashara, na kufanya  maamuzi ya siku zijazo kama "tatizo la mtu mwingine"  mawazo ambayo alielezea kuwa ya kutowajibika sana, ukosefu wa maadili, na kujishinda.

"Ujumbe wangu wa leo unatokana na hili: Usizingatie tu kile ambacho kinaweza kukutokea leo - na kuhangaika. Tazama kitakachotokea kwetu sote kesho - na uchukue hatua," mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema.

"Muda wa mabadiliko"

Jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuchukua hatua, aliendelea, kwa kuwa “huu si wakati wa kuchezea-chezea” bali, badala yake, “wakati wa mageuzi.”

Hatua zinapaswa kuzingatiwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa, hati iliyoanzisha shirika hili, na Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu, ambalo linatimiza miaka 75 mwaka huu.

"Ninapoangalia haki za binadamu kwa mapana zaidi - kwa lenzi ya karne ya 21 - naona ramani ya nje ya kuelekea mwisho mbaya," alisema, akibainisha kuwa lazima kuanzia kwenye kuzingatia haki ya amani.

Msichana mdogo wa Kiukreni akiwa amesimama kwenye vifusi vya shule yake iliyoharibiwa huko Zhytomyr.
© UNICEF/Diego Ibarra Sánchez
Msichana mdogo wa Kiukreni akiwa amesimama kwenye vifusi vya shule yake iliyoharibiwa huko Zhytomyr.

Fanya kazi kwa amani

Wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine Februari 24, 2022 ukisababisha mateso mengi kwa wakazi wa nchi hiyo, na hata wengine walio mbali zaidi, matarajio ya amani yanaendelea kupungua huku hatari ya kuongezeka zaidi na umwagaji damu ikiendelea kuongezeka.

"Ninahofia ulimwengu unaingia katika vita pana zaidi wakati ukiwa haujalala huku unatembea. Unafanya hivyo huku ukiwa macho wazi. Dunia inahitaji amani. Amani kulingana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa,” alisema na kuongeza kuwa "Lazima tufanye bidii zaidi kwa ajili ya amani kila mahali."

Bwana Guterres alirejelea hali ya Mashariki ya Kati, ambako suluhu ya mataifa mawili kati ya Palestina na Israel inazidi kuwa mbali; nchini Afghanistan, ambapo haki za wanawake zinakandamizwa; katika ukanda wa Sahel, ambako ukosefu wa usalama unaongezeka; nchini Myanmar, ambayo inakabiliwa na misururu mipya ya vurugu na ukandamizaji, na huko Haiti, ambapo ghasia za magenge zinashikilia nchi nzima.

Kujitolea tena kutimiza Mkataba wa Umoja wa Mataifa

"Ikiwa kila nchi itatimiza wajibu wake chini ya Mkataba hu, haki ya amani ingehakikishwa," alisema. "Ni wakati wa kubadilisha mtazamo wetu wa amani kwa kujitolea tena kuhakikisha tunatumiza matakwa ya Mkataba, kuweka haki za binadamu na utu mbele, kwa kujizuia moyoni mwetu."

Katibu Mkuu ametoa wito wa kuwepo kwa "mtazamo wa jumla wa mwendelezo wa amani" ambao unabainisha sababu kuu za migogoro na kuzingatia kuzuia, maridhiano, ujenzi wa amani na ushiriki mkubwa wa wanawake na vijana.

Hizi ni miongoni mwa Ajenda Mpya ya Amani inayopendekezwa na Umoja wa Mataifa, inayolenga kushughulikia vitisho vya zamani na vipya, na kuongeza miungano ya kidiplomasia, kama inavyothibitishwa na Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi ambao unafanya kazi hata wakati wa vita nchini Ukraine.

Hatari ya vita vya nyuklia

Katibu Mkuu Guterres amekumbusha mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 75 ya Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa, ambayo itashuhudia ongezeko la kujitolea kufanya mageuzi, ambapo ametoa wito kuwa suala linalopaswa kutiliwa mkazo ni kurejesha upokonyaji silaha na udhibiti wa silaha ili kupunguza vitisho vya kimkakati vya matumizi ya silaha za nyuklia na kufanya kazi ya kutokomeza kabisa.

"Tuko katika hatari kubwa zaidi katika miongo kadhaa ya vita vya nyuklia ambavyo vinaweza kuanza kama ajali au kubuni," alionya, akizitaka nchi zilizo na silaha za nyuklia kuachana na "silaha hizi zisizofaa".

Badilisha fedha za kimataifa

Huku umaskini na njaa zikiongezeka, nchi zinazoendelea zikizama katika madeni, na nyavu za usalama wa kijamii zikisambaratika, Katibu Mkuu alitoa wito wa "mabadiliko makubwa" ya usanifu wa fedha duniani.

Hili litahitaji kujitolea na azimio jipya, ikiwa ni pamoja na kushughulikia ukosefu wa usawa wa kutisha na ukosefu wa haki unaofichuliwa na janga la COVID-19 na mwitikio wa janga la kimataifa.

Azimio jipya pia litahitajika ili kuhakikisha nchi zinazoendelea zina sauti kubwa katika taasisi za fedha za kimataifa, na kwamba mataifa yaliyo hatarini, ikiwa ni pamoja na nchi za kipato cha kati, yanaweza kupata msamaha wa madeni na urekebishaji upya.

Benki za Maendeleo ya Kimataifa hasa, lazima zibadili mtindo wao wa biashara na kutumia fedha zao ili kuvutia mitaji zaidi ya kibinafsi ambayo inaweza kuwekezwa ili kusaidia nchi zinazoendelea kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kabla ya tarehe ya mwisho ya 2030.

"Bila ya mageuzi ya kimsingi, nchi tajiri zaidi na watu binafsi wataendelea kulundika mali, na kuacha makombo kwa jamii na nchi za Kusini mwa Ulimwengu," alionya mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.

Maendeleo endelevu katika hatari

Mwaka huu pia utatoa fursa za "kuokoa" SDGs, kama vile Mkutano wa Kilele wa Nchi Chini zinazoendelea (LDCs) mwezi ujao na mwingine mwezi Septemba unaolenga kuzingatia malengo hayo.

Huku SDGs tukiziona "zikitoweka kwenye kioo cha nyuma", nchi zinapaswa kuja kwenye mkutano huo zikiwa na vigezo vya wazi vya kukabiliana na umaskini na kutengwa, na mikakati ya kuendeleza usawa wa kijinsia.

Hata hivyo, dunia lazima iungane sasa kukusanya rasilimali, alisema Bw. Guterres, ili nchi zinazoendelea kiuchumi ziwe na ukwasi wa kuwekeza katika elimu, huduma za afya kwa wote, kujitayarisha kwa janga, kazi zenye staha na ulinzi wa kijamii.

Fundi anafanya kazi kwenye vifaa vya nishati ya upepo nchini Ufilipino.
© ADB/Al Benavente
Fundi anafanya kazi kwenye vifaa vya nishati ya upepo nchini Ufilipino.

Tuhesabu hatua za kuwa na hali ya hewa bora

Haki ya maendeleo inapokwenda pamoja na haki ya mazingira safi, yenye afya na endelevu, "lazima tukomeshe vita visivyo na huruma, visivyokoma, visivyo na maana dhidi ya asili," alisema Bw. Guterres, akirudia ujumbe ambao umekuwa kauli mbiu kwa muda wake. "2023 ni mwaka wa kufanya hesabu. Ni lazima uwe mwaka wa kuleta mabadiliko ya hali ya hewa. Tunahitaji kuvuruga mambo ili kukomesha uharibifu."

Nchi zinavuka kikomo cha nyuzi joto Sentigredi 1.5 duniani, kwa hivyo lazima kuzingatia vipaumbele vya haraka vya kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa na kufikia haki ya hali ya hewa.

Tuhamie kwenye nishati ya kijani

Alisema uzalishaji wa hewa ukaa duniani katika muongo huu lazima upunguzwe kwa nusu, ikiwa ni pamoja na kupitia "hatua kabambe zaidi" katika kuhama kutoka kwenye nishati ya mafuta kwenda kwa nishati mbadala, haswa katika kundi la G20 la mataifa yaliyoendelea kiviwanda.

Zaidi ya hayo, biashara, miji, mikoa na taasisi za kifedha ambazo zimeahidi kutoa hewa ukaa, lazima ziwasilishe mipango yao ya mpito, kwa malengo ya kuaminika na makubwa, kufikia Septemba hii.

"Nina ujumbe maalum kwa wazalishaji wa mafuta ya visukuku na viwezeshaji vyao vinavyojitahidi kupanua uzalishaji na kupata faida kubwa. Ikiwa huwezi kuweka dhamira ya kuaminika kwa net-zero, na malengo ya 2025 na 2030 yanahusu shughuli zako zote, hupaswi kuwa katika biashara," alisema Bw. Guterres.

Toani zile ahadi za COP27

Hatua za kupambana na mabadiliko ya tabianchi haziwezekani bila fedha, na Katibu Mkuu alizitaka nchi tajiri, angalau, kutekeleza ahadi zilizotolewa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP27 nchini Misri mwaka jana.

Ahadi hizi ni pamoja na kuanzisha hazina ya kushughulikia hasara na uharibifu, ufadhili wa kukabiliana na hali hiyo maradufu, na kuendeleza mipango ya mifumo ya tahadhari ya mapema duniani kote ndani ya miaka mitano ijayo.

Katibu Mkuu Guterres ataitisha Mkutano wa Wakuu w anchi kuhusu Mabadiliko ya tabianchi mwezi Septemba, kabla ya kongamano la COP28 litakalofanyika katika Umoja wa Falme za Kiarabu mwezi Desemba.

Itakuwa wazi kwa viongozi wote wa serikali, biashara na jamii, alisema, ingawa chini ya sharti moja: "Tuoneshe hatua za kasi katika muongo huu na kupanga upya mipango kabambe ya kufikia lengo la sifuri - au tafadhali usijitokeze."

Utofauti wetu unashambuliwa

Akigeukia kipaumbele chake cha nne, Bw. Guterres alizungumzia jinsi kuheshimu tofauti na usawa wa haki za kitamaduni kunavyoshambuliwa, kama inavyothibitishwa kwa sehemu na kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi, chuki dhidi ya Waislamu, mateso ya Wakristo, ubaguzi wa rangi na itikadi ya watu weupe.

Wakati huo huo, watu wachache wa ma kikabila na kidini, wakimbizi, wahamiaji, watu wa kiasili na jumuiya ya watu wa mapenzi ya jinsia moja LGBTQI-plus, wanazidi kulengwa kwa chuki, mtandaoni na nje ya nchi.

Wakati huo huo, watu wengi walio katika nyadhifa za madaraka wananufaika kutokana na kuiga aina mbalimbali kama tishio, kupanda migawanyiko na chuki, huku majukwaa ya mitandao ya kijamii yanatumia kanuni za algorism zinazokuza mawazo yenye sumu na kuleta maoni yenye itikadi kali katika jamii kuu.

Serikali na makampuni ya intaneti wameshindwa kuzuia chuki mtandaoni
Unsplash/Priscilla du Preez
Serikali na makampuni ya intaneti wameshindwa kuzuia chuki mtandaoni

Kupambana na chuki mtandaoni

Katibu Mkuu alisisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kulinda haki za kitamaduni na tofauti, ikiwa ni pamoja na kupitia mipango ya mauaji ya Holocaust na Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda, pamoja na Mkakati na Mpango wake wa Utekelezaji wa Matamshi ya Chuki.

"Tutaomba hatua zichukuliwe kutoka kwa kila mtu aliye na ushawishi katika kuenea kwa taarifa potofu na zisizo sahihi kwenye mtandao Serikali, wadhibiti, watunga sera, makampuni ya teknolojia, vyombo vya habari, mashirika ya kiraia," alisema.

“Acheni chuki. Weka vituo vikali vya ulinzi. Uwajibike kwa lugha inayoleta madhara.”

Mfumo dume unarudisha mambo nyuma

Huku nusu ya ubinadamu "ikizuiliwa na unyanyasaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu wa wakati wetu," mkuu wa Umoja wa Mataifa alisisitiza haki ya usawa kamili wa kijinsia.

Alisisitiza hasa masahibu ya wanawake na wasichana nchini Afghanistan, sasa "walio uhamishoni katika nchi yao" kutokana na sheria zinazowapiga marufuku kufurahia maisha ya umma.

Ubaguzi wa kijinsia ni wa kimataifa, alisema, na mambo yanazidi kuwa mabaya.

"Tunakabiliwa na msukumo mkali dhidi ya haki za wanawake na wasichana. Haki za wanawake za kujamiiana na uzazi na ulinzi wa kisheria uko chini ya tishio. Katika ngazi ya kimataifa, baadhi ya serikali sasa zinapinga hata kuingizwa kwa mtazamo wa kijinsia katika mazungumzo ya pande nyingi,” alisema.

Usawa wa kijinsia kimsingi ni suala la madaraka, na mfumo dume unajiimarisha, alisema, lakini Umoja wa Mataifa unapigana na kusimama kwa ajili ya haki za wanawake na wasichana kila mahali, ikiwa ni pamoja na katika safu zake.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia aliahidi "kupunguza maradufu" na kuongeza juhudi za uungwaji mkono wa hatua za kuelekea usawa zaidi wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na mgawo wa kuziba mapengo katika uwakilishi wa wanawake, katika uchaguzi, vyumba vya bodi za mashirika na mazungumzo ya amani.

‘Janga’ la ukiukaji wa haki

Wakati huo huo, haki za kiraia na kisiasa ambazo ni msingi wa jamii-jumuishi pia ziko chini ya tishio, kwani demokrasia inarudi nyuma.

"Gonjwa hili lilitumika kama kifuniko cha janga la ukiukaji wa haki za kiraia na kisiasa," Bwana Guterres alisema, akionya kwamba nafasi ya kiraia "inatoweka mbele ya macho yetu".

Aliripoti kuhusu vitisho kama vile sheria kandamizi zinazozuia uhuru wa kujieleza, teknolojia mpya ambazo hutumika kama kivuli cha kudhibiti uhuru wa kukusanyika au hata kutembea, na ongezeko la mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari.

Kupitia Wito wa Katibu Mkuu wa Kuchukua Hatua kwa Haki za Binadamu, Umoja wa Mataifa unajitahidi kuendeleza uhuru wa kimsingi, kukuza ushiriki wa mashirika ya kiraia, na kulinda nafasi ya kiraia duniani kote.

"Na tunaimarisha uungaji mkono wetu kwa sheria na sera zinazolinda haki ya ushiriki na haki ya uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari huru na huru," aliongeza.

Katibu Mkuu António Guterres akiwa na wanaharakati vijana wa hali ya hewa katika Mkutano wa Utekelezaji wa Hali ya Hewa huko COP27 huko Sharm el-Sheikh, Misri.
UNFCCC/Kiara Worth
Katibu Mkuu António Guterres akiwa na wanaharakati vijana wa hali ya hewa katika Mkutano wa Utekelezaji wa Hali ya Hewa huko COP27 huko Sharm el-Sheikh, Misri.

Tushirikishe vijana

Katibu Mkuu alisisitiza kwamba vitisho vinavyohujumu haki leo pia vitakuwa na athari kwa vizazi vijavyo, ambavyo mara nyingi huchukuliwa kuwa ni jambo la kawaida tu.

Alionesha matumaini kwamba Mkutano Mkuu wa kizazi kijacho, uliopangwa kufanyika mwaka ujao, utaleta haki hizi mbele ya majadiliano ya kimataifa.

"Hakuna eneo bunge kubwa zaidi la kutetea mustakabali huo kuliko vijana - na Ofisi mpya ya Umoja wa Mataifa ya Vijana ambayo itakuwa na uendeshaji mwaka huu imeundwa ili kuimarisha kazi yetu," alisema.

Juhudi hizi pia ni fursa ya kuongeza hatua za kimataifa na kujenga Umoja wa Mataifa ambao unafaa kwa enzi mpya, aliongeza.