Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na wadau kuongeza wigo wa vyanzo vya maji Somalia

Picha: UM/Video capture
Bwawa la maji.

FAO na wadau kuongeza wigo wa vyanzo vya maji Somalia

Tabianchi na mazingira

Shirika la chakula kilimo na duniani FAO, kwa ushirikiano mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu, lile la maji, usafi na mazingira (WASH Cluster ) na la mazingira kutoka serikali ya Norway (Yme/GSA ) wameandaa warsha yenye lengo la kutoa muongozo kuhusu upanuzi wa mradi mpya wa maji kwa kutumia vyanzo vya  maji ya chini ya ardhi nchini Somalia.

Warsha hiyo, imejumuisha watalamu kutoka SWALIM ambayo ni  idara ya uchunguzi wa vyanzo vya maji Somalia na baadhi ya viongozi kutoka wizara ya nishati na maji nchini humo.

Dr. Abdullahi Elmi Mohamedkutoka kituo cha maji na mazingira nchini Somalia amesifu jitihada za idara ya uchunguzi wa  vyanzo vya maji SWALIM kwa kuweza kuisaidia serikali ya Somalia kwa ujumla katika kufanya uchunguzi wa vyanzo vya maji kwa muda mrefu.

Idara ya SWALIM kwa ushirkiano na FAO wamsema wataendelea kutoa msaada wa  kitaalamu katika miradi ya upanuzi wa vyanzo vya maji Somalia ili kufikia hatua ya kuwa na mradi endelevu wa maji kwa wananchi wa Somalia  taifa ambalo mara nyingi linakumbwa na matatizo ya ukame na uhaba mkubwa wa maji..