Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuliona fursa katika kuchakata taka na hatukusita tukaichangamkia: Greencare Rwanda

Green Care nchini Rwanda imekuja na suluhisho endelevu la kukusanya taka nchini humo.
UN/Flora Nducha
Green Care nchini Rwanda imekuja na suluhisho endelevu la kukusanya taka nchini humo.

Tuliona fursa katika kuchakata taka na hatukusita tukaichangamkia: Greencare Rwanda

Tabianchi na mazingira

Taka zinazotupwa hivyo bila utaratibu maalum wa kuzidhibiti  ni mtihani mkubwa kwa jamii nyingo hususan barani Afrika na kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa athari zake ni mbaya kiafa na kimazingira. Lakini vijana katika wilaya ya Huye iliyoko jimbo la Kusini mwa Rwanda hawakuona athari tuu za kiafya au mazingira katika kudhibiti taka hizo bali waliona fursa pia hasa za ajira na kiuchumi, ndipo walipoamua kulivalia njuga sula hilo na kuanzisha mradi wa Green care  

Soundcloud

Mradi wa Greencare Rwanda ulianza mwaka 2016 na ulioanzishwa na vijana wanne wajasiriliamali ambao walihitumu shada zao kwenye chou kikuu cha Rwanda mwaka 2015 Noel Nizeyimana ambaye ndiye mkurugenzi mtendaji au CEO na wenzie Francis Mizinduko, Christian Ruzindana, and Jean Paul Iyakaremye.  

Baada ya kuhangaika mwaka mzima kusaka ajira bila mafanikio ndipo walipobaini fursa kwenye taka zilizokuwa zimetapakaa kila kona ya wilaya yao ya Huye. Agent Mugwaneza ni afisa operesheni wa mradi huo afafanua leo kuu la kuanzishwa mradi huo “Ni kutoa suluhu jumuishi za usimamizi wa taka, kilimo endelevu  kupitia uchagizaji na uzalishaji wa mbole asilia. Wakati huo wa 2016 hakukuwa nae neo maalum au damo la kutupa taka, kulikuwa nae neo dogo tu nje ya mji, taka zilikuwa zinachomwa na ilikuwa inasababisha athari za kiafya na kimazingira. Hivyo baada ya kuhitimu Rwanda tukaona hiyo ni fursa ya biashara kw akua asilimia kubwa ya taka hizo ni za asili na zinaweza kugeuzwa kuwa mbolea”. 

Mradi umekwamua vijana

Pia mradi huo umesaidia sana vijana hao na wengine waliowaajiri kujikwamua kiuchumi huku wakilinda na kuhifadhi mazingira yanayowazunguka. 

Agneta akaendelea kunieleza wanachokifanya baada ya kukusanya taka hizo kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Huye “Tunachokifanya ni usimamizi wa taka, na tunabadili sehemu ya taka hizo kuwa mbolea asilia na sehemu t ya taka zingine ambazo sio asili kama plastiki tunazichakata na kutengezeza matofali ya lami” 

Wafanyakazi wa Green Care nchini Rwanda wakiwa kwenye dampo. Kampuni hii imejikita katika udhibiti wa taka na kutengeneza mboji au samadi.
UN/ Flora Nducha
Wafanyakazi wa Green Care nchini Rwanda wakiwa kwenye dampo. Kampuni hii imejikita katika udhibiti wa taka na kutengeneza mboji au samadi.

Taka wanazozichakata hapa zinatoka katika wilaya nzima ya Huye na kwa kutambua mchango wao katika kuhifadhi mazingira shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP Rwanda tarehe 5 Juni 2021 siku ya mazingira duniani liliutunukia tuzo ya ubunifu na uwekezaji mradi wa Greencare tuzo iliyoambatana na cheki ya Franc za Rwanda milioni 6 sawa na dola 6000 za Marekani likisema ni mfano bora wa kuigwa katika usimamizi endelevu wa taka. 

Mradi ulipigwa jeki kwa kweli - Agneta

Agneta anasema fedha hizo zilisaidia sana katika mafanikio ya mradi huo ikiwemo 

“Tunatoa fursa za ajira kwa vijana na wanawake na pia tunachangia katika uzalishaji wa mbolea ya asili ambayo inahitajika sana na wakulima na kuhusu mazingira tumeweza kudhibito hatari za kimazingira zinazosababishwa na kutodhibiti taka.” 

Mbali ya wakulima wadogowadogo wa Huye Agneta anasema wateja wao wakumbwa ni makampuni makubwa yanayohusika na kilimo asilia, masoko ya bidhaa za kilimo, na vyma vya ushirika. 

Na kwa viajana waanzolishi wa mradi wa Greencare wanasema mradi huu umekuwa ni ushidi mkubwa sio tu kwa kuwatatulia tatizo la ajira bali pia kuwainua vijana wenzao na wanawake wa Huye kwani hadi kufikia sasa wameshaajiri vijana na wanawake 21 na hivyo kuziinua kiuchumi familia zao na kuchangia katika maendeleo ya jamii.