Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yakaribisha uamuzi wa Marekani kupokea wakimbizi 125,000

Kituo cha mpito nchini Zambia chawezesha wakimbizi wa nchi jirani kurejea nyumbani bila kuhangaika. Picha: IOM

UNHCR yakaribisha uamuzi wa Marekani kupokea wakimbizi 125,000

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na wakimbizi UNHCR limekaribisha taarifa la Marekani kuwa kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2022 ambayo ni mwanzo wa mwaka mpya wa fedha wa nchi hiyo  watachukua wakimbizi 125,000 wanaohamia Marekani kama nchi ya tatu.

 

wakilishi wa UNHCR katika nchi ya Marekani n anchi za Karibiani, Matthew Reynolds katika taarifa yake kwa umma ameishukuru Marekani kwa uamuzi huo wa kuchukua wakimbizi na kusema Shirika hilo lipo tayari kushirikiana na serikali, asasi za kiraia, wakimbizi wenyewe na watu wengine wote watakao husika katika mchakato mzima ili kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu mchakato mzima wa kuwaleta wakimbizi hao Marekani

Reynolds amesema “Kuwaleta wakimbizi Marekani kunatoa fursa kwa wakimbizi ambao wengine wapo katika maeneo hatarishi duniani na kutawawezesha kujenga upya maisha yao kwa amani na staha hapa Marekani baada ya kuyakimbia makazi yao”.

Ameongeza kuwa uamuzi huo wa Marekani ni uthibitisho wa huruma kwa watu wenye uhitaji wa ulinzi ili kuokoa Maisha yao ambao serikali na watu wa Marekani wanao kwa miaka mingi na inajulikana wazi.

“Pia unatoa kama mfano rahisi na thabiti kwa kutafsiri kanuni za kibinadamu kuwa sera kwa wengine kufuata”, alisema Mwakilishi huyo wa UNHCR wakati akihitimisha taarifa yake.