Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angela Merkel ashinda tuzo ya UNHCR ya Nansen kwa mwaka 2022

Dkt. Angela Merkel, Kansela wa zamani wa Ujerumani, atapokea Tuzo la Wakimbizi la UNHCR la Nansen la 2022.
© Bundesregierung/Steffen Kugler
Dkt. Angela Merkel, Kansela wa zamani wa Ujerumani, atapokea Tuzo la Wakimbizi la UNHCR la Nansen la 2022.

Angela Merkel ashinda tuzo ya UNHCR ya Nansen kwa mwaka 2022

Haki za binadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limemtangaza aliyekuwa Kansela wa Ujerumani Angela Maerkel kuwa ni mshindi wa tuzo ya wakimbizi ya Nansen kwa mwaka 2022 kutokana na mchango wake wa kusaidia wakimbizi kutoka Syria wakati machafuko yaliposhika kasi nchini mwao. 

Kila mwaka tuzo hii hutolewa kwa mtu, kikundi au shirika ambalo limefanya juhudi kubwa kuhakikisha wakimbizi wanalindwa, kuwasaidia wakimbizi wa ndani na wale wasio na utaifa. 

Tuzo ya Nansen imetolewa kwa Merkel kwa kuwa chini ya uongozi wake, Ujerumani ilikaribisha wakimbizi zaidi ya milioni 1.5 wengi wao wakikimbia mzozo mkali nchini Syria na maeneo megine. 

Katika kipindi hicho Merkel alinukuliwa akisema “Ilikuwa hali ambayoilikuwa inatujaribu maadili yetu ya ulaya mara chache hapo awali. Haikuwa zaidi na pungufu zaidi ya kuangalira sharti la kibinadamu.” Alisema hayo na kutoa wito kwa Wajerumani wenzake kukataa utaifa unaoleta mgawanyiko na kuwataka badala yake "kujiamini, kuwa huru, wenye huruma na wenye nia wazi".

Kupitia taarifa yake kutoka Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa wakimbizi Filippo Grandi, alimpongeza Kansela huyo wa zamani wa Ujerumani Merkel kwa azma yake ya kuwalinda wanaotafuta hifadhi na kutetea haki za binadamu, kanuni za kibinadamu na sheria za kimataifa. "Kwa kuwasaidia zaidi ya wakimbizi milioni moja kuishi na kujenga upya maisha yao, Angela Merkel alionesha ujasiri mkubwa wa kimaadili na kisiasa," alisema Grandi.

Mkuu huyo wa UNHCR amesema kamati ya uteuzi imefikia uamuzi wa kutoa tuzo kwa Kansela Merkel kwakuwa imetambua uongozi wake, ujasiri wake na huruma katika kuhakikisha mamia ya maelfu ya watu waliokata tamaa huku wakisaidia kupata suluhu za muda mrefu.

Kamishna wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel ameshinda tuzo ya Nansen ya UNHCR
© Bundesregierung/Steffen Kugler
Kamishna wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel ameshinda tuzo ya Nansen ya UNHCR

Washindi wa kikanda

Kamati hiyo pamoja na kutoa tuzo ya Nansen kwa Merkel pia imetangaza washindi wanne wa kikanda duniani kwa mwaka huu 2022.

Kutoka barani Afrika, Mshindi ni kikosi cha zimamto cha Mbere cha nchini Mauritania ambapo wafanyakazi wake ni wakimbizi wanaojitolea katika kuzima moto wa nyika na wameshazima zaidi ya mara 100. Pia kikundi hicho kinapanda mitin a kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.

Kutoka bara la Amerika, Vicenta González, ambaye kwa takriban miaka 50 amekuwa akihudumia watu wanaoyakimbia makazi yao na wakiishi katika magumu. Vicenta alianzisha ushirika wa kakao nchini Costa Rica ili kusaidia wakimbizi na wanawake wa jumuiya zinazowahifadhi, ikiwa ni pamoja na manusura wa unyanyasaji wa nyumbani.

Kutoka Asia na Pasifiki, tuzo imeenda kwa Meikswe Myanmar, hili ni shirika la kibinadamu linalosaidia jamii za wahitaji ikiwa ni pamoja na kuwapatia mahitaji ya dharura, huduma za afya, elimu, na fursa za kujikimu.

Na Tuzo nyingine ya eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, imeenda kwa Dk. Nagham Hasan, Daktari wa magonjwa ya wanawake raia wa Iraq ambaye amekuwa akitoa huduma za matibabu na kisaikolojia kwa wasichana na wanawake wa Yazidi ambao walinusurika mateso, utumwa na unyanyasaji wa kijinsia kutoka mikononi mwa vikundi vya itikadi kali kaskazini mwa Iraq.

Tuzo hiyo kwa Kansela Merkel na washindi wengine wa kikanda itatolewa jijini Geneva, Uswisi tarehe 10 Oktoba katika sherehe ya pamoja.

Rosa, mwenyeji wa Boruca kutoka Costa Rica
Rosa Fernández
Rosa, mwenyeji wa Boruca kutoka Costa Rica

Kuhusu tuzo ya Nansen

Kila mwaka, tuzo hiyo iliyopewa jina la mgunduzi wa Norway, mwanasayansi, mwanadiplomasia na msaidizi wa kibinadamu Fridtjof Nansen, hutolewa kwa mtu binafsi, kikundi au shirika ambalo limefanya juhudi  za kulinda wakimbizi, wakimbizi wa ndani au watu wasio na utaifa.

Mwaka huu UNHCR wanaadhimisha karne moja tangu Fridtjof Nansen, Kamishna Mkuu wa kwanza wa Wakimbizi alipo tunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 1922 kwa juhudi zake za kuwarudisha nyumbani wafungwa wa vita na kulinda mamilioni ya wakimbizi waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro, mapinduzi na kuanguka kwa Romanov, Ottoman na Milki ya Austro, Hungarian.

Pia ni miaka 100 tangu kuundwa kwa pasipoti ya Nansen, hati ya utambulisho kwa wakimbizi, wengi wao wasio na uraia, ambayo pia iliwezesha wamiliki wake kuvuka mipaka kutafuta kazi.