Mswada wa Uingereza wa kutuma waomba hifadhi nchini Rwanda ‘unaenda kinyume na haki za binadamu’: Volker Türk
Hatua ya bunge la Uingereza kuwezesha kuondolewa mara moja kwa waomba hifadhi kupelekwa nchini Rwanda inaenda kinyume na kanuni za msingi za utawala wa sheria na hatari ya kutoa “pigo kubwa” kwa haki za binadamu, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameonya hii leo.