Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupigania haki za binadamu ni jukumu linaloendelea: Bachelet

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet akiwa ziarani nchini Nigeria
© OHCHR/Anthony Headley
Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet akiwa ziarani nchini Nigeria

Kupigania haki za binadamu ni jukumu linaloendelea: Bachelet

Haki za binadamu

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet anahitimisha muhula wake mamlakani kesho Jumatano 31 Agosti baada ya kuhudumu katika wadhifa huo kwa miaka minne.

Kabla ya kukabidhi kijiti cha jukumu hilo alipata fursa ya kuketi na UN News kutathimini yaliyojiti katika wakati wa uongozi wake zikiwemo changamoto, mafanikio na matarajio.

Pia akarejea alichokisema wakati akipokea kijiti hicho miaka minne iliyopita kwamba kupigania haki za binadamu ni mzunguko usio na mwisho “ Ni kazi ambayo haina mwisho, kwa hivyo labda kuna mambo mengi ambayo hatukuweza kufanya au kufikia, kwa sababu sio kitu ambacho unaweza kufanikiwa kama, namaanisha kwa mfano, wengi wetu, sio sisi tu, lakini bila shaka na, pamoja na mashirika ya kiraia, na mashirika mengine, tumekuwa na baadhi ya hatua muhimu za kufanyika, mfano, uamuzi wa Baraza Kuu, kwamba kuna haki ya binadamu - haki ya mazingira yenye afya, na mapambano dhidi ya uchafuzi wa mazingira, na kadhalika. Na haya yalikuwa mapambano ya muda mrefu kutoka kwa mashirika ya kiraia, lakini baadaye ushirikiano mkubwa kati yetu na WHO, kusukuma ajenda hiyo. Na kisha kukawa na azimio la Baraza la Haki za Kibinadamu, ambalo lilienda kwenye Baraza Kuu na naweza kusema, liliidhinishwa na wengi au idadi kubwa. Kwa hivyo, nadhani hiyo ilikuwa muhimu sana.”

Hata hivyo Bi. Bachelet anasema bado anaamini kwamba tishio kubwa la haki za binadamu linajikita katika mambo matatu “Ninaamini kwamba tishio baya zaidi kwa wanadamu ni kile tunachoita majanga matatu ya sayari hii ambayo ni mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira na upotevu wa viumbe hai. Kwa hivyo, azimio hili shukrani kwa mkataba wa Paris na nchi wanachama kuchukua hatua kwa vitendo, nadhani itakuwa hatua muhimu sana.”

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Michelle Bachelet akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva
© OHCHR/Anthony Headley
Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Michelle Bachelet akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva

Kuna mafanikio tuliyopiga

Mkuu huyo wa haki za binadamu amesema Pamoja na changamoto hizo kubwa kuna matumaini "Tumepata vitu vingine, naweza sema tumeona mienendo fulani kuelekea kukomesha hukumu ya kifo kwani sasa zaidi ya nchi 170 aidha zimepiga marufuku, au zimeanzisha mchakato wa kusitisha hukumu ya kifo na nchi zaidi zimetangaza kwamba zitaenda katika mwelekeo huo huo. Hiyo nadhani ni habari njema sana pia.”

Ameongeza kuwa katika baadhi ya maeneo wameweza kusaidia wat una hivyo sauti zao zimesikika na sheria zikaweza kubadilishwa kwa faida ya walio wengi “Hasa kwa upande wa kulinda na kuchagiza haki za binadamu za wanawake au watoto. Pia naweza kusema kwamba tumekuwa katika mchakato wa kulinda haki wa watetezi wa halki za binadamu.”

Masuala mengine ambayo amehakikisha yanafanmyiwa kazi amesema ni pamoja na kusaidia makubaliano ya Escazu kwa ushirikiano na ECLAC Amerika ya Kusini ambao ni mkataba wa kwanza ambao unahoji umuhimu wa ushiriki wa watu katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi lakini pia kulinda watetezi wanaopigania haki za mazingira iwe ni kwa watu wa asili au watetezi wa masuala ya ardhi.

“Hiyvo kumekuwa na mambo makubwa kama hayo lakini pia madogo katika kila nchi tunapoweza kuzungumza na serikali kusaidia asasi za kiraia kubadili sheria fulanifulani au kuzuia baadhi ya miswada kupitishwa mambo yanaweza kwenda kombo. Lakini ni kazi ambayo ina malengo makubwa, ya kati na madogo kwa sababu unahitajika kufanya mambo mengi tofauti kwa sababu ni maeneo mengi. Kwa mantiki hiyo tunahitaji kuendelea kufanya kazi na endapo Kamisha yeyote atasema kila kitu kimefanyika nitasema la hasa hiyo sio hali halisi.”

Kamisha Mkuu wa Haki za binadamu wa Un Michelle Bachelet alipokutana na kijana mwanaharakati Greta Thunberg wakati wa COP25 Madrid mwaka 2019
© OHCHR/Anthony Headley
Kamisha Mkuu wa Haki za binadamu wa Un Michelle Bachelet alipokutana na kijana mwanaharakati Greta Thunberg wakati wa COP25 Madrid mwaka 2019

Mabadiliko katika kmwelekeo wa haki za binadamu

Kamishina mkuu amesema katika miaka minne aliyokuwa madarakani kumekuwa na mambo mengi yaliyojitokeza

” Kweli, ulimwengu umebadilika sana ningesema kwa miaka minne, janga, na athari inayoongezeka ya mabadiliko ya tabianchi. Na sasa tunaona mishtuko inayorejea ya mzozo wa chakula, mafuta na fedha kama matokeo ya vita vya Ukraine. Tumeona pia mgawanyiko mkubwa katika ngazi ya kimataifa, na pia tumeona vuguvugu la maandamano na mapinduzi ya kijeshi huko Myanmar, Burkina Faso, Guinea na Mali, na pia kuchukuliwa madaraka na Taliban nchini Afghanistan. Na kwa hivyo ningesema hili sio jambo linaloenda upande mmoja tu, kwa sababu upande mmoja, ndio, unaweza kuona mambo mengi ambayo yanaenda vibaya na hayasaidii haki za binadamu."

Pamoja na hayo ametaja janga la coronavirus">COVID-19 ambapo imeshuhudiwa katika baadhi ya nchi wakitumia vikwazo kwa sababu za kiafya. “Wanaamua kubinya uhuru wa vyombo vya Habari jambo ambalo sio la lazima kukabiliana na janga la coronavirus">COVID-19. Lakini kwa upande mwingine naweza kusema sio mtu ninayehisi kwamba  hiki ni kitu kisichoweza kubadilika , kwa upande mmoja hatuwezi kulichukulia kwa mzaha kwa sababu hakuna aliyedhani vita mpya itazuka barani Ulaya , na sasa tunayo na tulidhani kwamba haki za binadamu ni kawaida na kumbe sivyo. Na tumeshuhudia kwamba nchi ambazo kila wakati zunazungumzia haki za binadamu haimanishi kwamba zinaheshiku haki hizo kila wakati.”

Kamisha Mkuu wa haki za binadamu Michelle Bachelet akiwa ziarani Burkina Faso
© OHCHR/Anthony Headley
Kamisha Mkuu wa haki za binadamu Michelle Bachelet akiwa ziarani Burkina Faso

Ni mapambano ya kila wakati

Bachet ameongeza kuwa kudumishja haki za binadamu “Ningesema ni mapambano ya kudumu na yasiyo na mwisho sio tu kufahamu, bali kutoa wito kwa nchi wanachama kuendelea (na jukumu lake) ambalo ni kulinda na kukuza haki za binadamu, na pia kusaidia asasi za kiraia ili zifanye sehemu yao pia. Lakini kwa upande mwingine, umeona vuguvugu nyingi muhimu, vijana wakiandamana kwa ajili ya sayari hii, wanawake, kampeni ya Me Too au, Black Lives Matter na maandamano yote ya kuunga mkono kukomesha ubaguzi wa kimfumo, na kadhalika. Kwa hivyo, ningesema kumekuwa na (a)kuzorota katika baadhi ya maeneo, lakini kwa upande mwingine, kumekuwa na hatua muhimu zilizopigwa. Kwa hivyo kama kawaida maishani, una wakati mzuri na wakati mgumu, na lazima ufanye kazi na nyakati zote mbili.”

 

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu Michelle Bachelet akiwa ziarani Bunia Congo DRC
© OHCHR/Anthony Headley
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu Michelle Bachelet akiwa ziarani Bunia Congo DRC

Kinachopaswa kuendelea kufanyika

Kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea katika maeneo yenye migogoro kama Ukraine, Yemen na Tigray Ethiopia Bi. Bachelet amesema angependa kuona “Kazi inaendelea kufanyika masuala yote haya lakini ningependa jumuiya ya kimataifa isisahau kuhusu hali hizo, na wakati mwingine kwa sababu mambo mengi ni katika ajenda na baadhi ya mambo kuchukua umuhimu zaidi katika vyombo vya habari kuzungumza kisiasa, ni kwamba baadhi yao hasa juu ya migogoro ya muda mrefu, nahisi imesahaulika, na watu wanahisi kuachwa na jumuiya ya kimataifa. Kwa mfano, tunaona huko Yemen kwamba licha ya suluhu kuna ukiukwaji mkubwa unaoendelea.”